SAFARI ya Janette na mama yake imekuwa ikiandamwa na mikosi na upinzani mkali tangu walipotoroka kambi ya jeshi la waasi. Baada ya kutoka salama mjini Zombo, wanakutana na mtihani mwingine katika msitu wa Zombo.
Baada ya mapambano makali ya silaha katika msitu wa Zongo, hatimaye Janette na mama yake wamefanikiwa kuvuka salama na kufika mpaka wa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Afrika ya kati. Wakati huo Janette hali yake ni mbaya baada ya kujitonesha bega wakati wa mapigano. Nini hatima ya safari yake na jeraha? Je, watavuka salama? Ili kujua
BAADA ya kuachana na dereva, kijana aliyeletwa kwa ajili ya kuwavusha mpakani aliwaeleza wamfuate. Walikwenda pembeni kidogo kwenye maduka na soko dogo kulipokuwa na bodaboda nyingi. Walichukua bodaboda tatu na kuelekea sehemu ambayo alikuwa akiijua mwenyeji wao.
Baada ya kwenda kwa dakika kumi na tano walifika sehemu hiyo. Ilikuwa nje kidogo ya Mji wa Bangassou ambako kulikuwa na uzio wa chuma (Seng’enge) pembeni ya miti mingi. Madereva wa bodaboda walilipwa na kuondoka kuwaacha Janette na mama yake na mwenyeji. Walisogea kwa mbele na kuingia kwenye vichaka pembeni ya uzio ule.

Muda wote Janette alikuwa akijiuliza watapita wapi ikiwa uzio ule wa chuma ulikuwa umezunguka sehemu kubwa. Waliacha njia ya miguu na kuingia kwenye korongo moja ambalo walitembea kwa dakika tano na kutokea sehemu moja iliyoonyesha imechimbwa kwa chini na kunyanyuliwa seng’enge.
“Hii ndiyo njia yetu,” alisema mwenyeji wao.
“Hakuna tatizo.”

Walianza kuingiza mizigo kwanza kisha walifuata mmoja mmoja mpaka wakaingia wote. Waliingia ndani ya uzio sehemu iliyokuwa na miti mingi kumaanisha wamo ndani ya Nchi ya Afrika ya Kati nje kidogo ya Mji wa Bangassou. Mwenyeji alitangulia mbele akiwa amebeba begi la wateja begani na nyuma walifuata Janette na mama yake.
Walitembea kwa zaidi ya saa nzima na kutokea sehemu yenye barabara kuu, muda huo giza lilikuwa limeishaingia. Walisimama kwa nusu saa, baadaye ilipita pick up iliyokuwa imebeba mizigo ambayo waliisimamisha. Iliposimama mwenyeji aliwaeleza sehemu wanayokwenda. Mwenyeji na mama Janette walikaa nyuma kwenye mizigo, Janette kwa vile alikuwa mgonjwa alikaa mbele. Safari iliendelea kwa muda wa nusu saa na kuingia mjini Bangassou majira ya saa mbili usiku.
Baada ya kumlipa mwenye pick up, mwenyeji wao aliwaeleza wamfuate, kwa vile Janette asingeweza kwenda safari ndefu bila kupata matibabu ilibidi apelekwe kwenye hospitali ya kulipia.
Mwenyeji wao aliyefahamika kwa jina la Ras kutokana na kusokota nywele zake, aliwatafutia hospitali ambayo alikuwa akiitumia hasa alipokuwa na wazamiaji wake waliokuwa wakiingia nchini bila pasipoti pale walipokuwa hali zao siyo nzuri. Baada ya kukutana na daktari ambaye hakutaka kuhoji mambo mengine zaidi ya kutoa huduma, Janette alipewa huduma mara moja.

Mama Janette na Ras walikaa kwenye nyumba ya wageni ya Uswahilini ya bei nafuu, kwa vile alikuwa safarini hakujali kitu. Janette alipata huduma nzuri na kupewa vidonge vya kupunguza maumivu haraka na kupata mapumziko ya siku mbili kama alivyoomba.
Baada ya kukaa Bangassou kwa siku mbili, siku ya tatu walianza safari ya kuizunguka Jamhuri ya

Kidemokrasia ya Kongo kupitia nchini ya Afrika ya Kati mpaka Sudani ya Kusini. Ilibidi watumie usafiri wa kawaida ambao hakuna aliyekuwa akimchunguza mtu yeyote aliyekuwa akisafiri ndani ya nchi.
Walikata tiketi ya basi lililokuwa likielekea Mji wa Rifai, safari ilianza saa kumi na mbili alfajiri. Ulikuwa umbali mrefu sana, walifika Mji wa Rifai saa nne usiku, kwa vile safari ilikuwa ikiendelea Ras alitoa wazo.
“Jamani kwa vile safari bado mbichi, hakuna umuhimu wa kupoteza fedha bila sababu, nilikuwa nashauri tusitafute nyumba ya wageni bali tulale hapahapa kituoni kwa vile alifajiri tutaendea na safari.”
“Hakuna tatizo tunakusikiliza wewe,” alijibu Janette.

Baada ya kupata chakula hawakuwa na haja ya kuoga, walilala palepale kituo cha mabasi cha Mji wa Rifai mpaka alfajiri ambapo walipanda basi dogo lililokuwa likiishia mji mdogo wa Zemio.
Safari iliendelea, ilikuwa umbali kama kutoka jijini Dar es salaam mpaka Dodoma, ilichukua saa sita. Lakini kutokana na ubovu wa barabara, walifika Mji wa Zemio alasiri saa tisa. Ras hakupenda kufika muda ule kwa vile alipanga waunganishe mpaka Mji wa Mboki ambao kama wangefika saa kumi na moja jioni, wangeweza kuunganisha mpaka Mji wa Obo ambako ndipo wangelala mpaka siku ya pili kuelekea Mji wa Riyubu mji ulio mpakani mwa Nchi ya Sudani na Afrika ya Kati.Kwa vile walifika Mji wa Zemio saa tisa alasiri, Ras aliwashauri wakalale Mji wa Mboki ili kesho waendelee na safari. Janette na mama yake hawakuwa na neno zaidi ya kumsikiliza mwenyeji wao. Hakukuwa na haja ya kula zaidi ya kununua vyakula laini vya kula safarini.

Walifika Mji wa Mboki majira ya saa mbili usiku na kutafuta nyumba ya wageni kulala kwa vile walikuwa wamechoka sana pia kulipumzisha jeraha la Janette ambalo halikutakiwa kupata msukosuko kwa muda mrefu.
Walitafuta hoteli iliyokuwa karibu na kituo cha basi na kulala ili kesho asubuhi waendelee na safari. Walipumzika mpaka siku ya pili walipoanza safari yao ya kuelekea Mji wa Obo.
Ras aliamini kama safari itaenda vizuri basi wangefika saa moja usiku mpakani na kufanya mchakato usiku uleule kuingia Sudani ya Kusini ili asubuhi waanze safari ya kuelekea Uganda.

Safari ilianza saa mbili asubuhi kutokana na gari walilokata tiketi kuwa na matatizo na kufanyiwa matengenezo. Safari ilianza lakini baada ya kutembea kwa saa sita liliharibika tena. Lilitengenezwa kwa saa mbili na safari iliendelea, kutokana na ubovu wa gari ilibidi kwenda taratibu.
Lakini halikutembea sana liliharibika tena, kutokana na kuonekana tatizo kubwa ilibidi abiria wateremke tena na kukaa pembeni kusubiri mpaka litengenezwe. Gari ilionekana lina tatizo kubwa, ilibidi waombe msaada wa kifaa kilichoharibika kiletwe kutoka mjini Mboki.
Kwa hesabu ya haraka ilibidi waongeze saa sita mpaka nane ndipo gari kutoka mjini lifikie eneo la tukio kuleta spea iliyoharibika. Kwa hiyo ilionyesha mpaka saa kumi na mbili au saa moja usiku ndipo kifaa kifike na matengenezo yalionyesha yatakuwa saa nne usiku.
Sehemu waliyokuwepo ilikuwa mbuga tupu lakini kwa mbele kama umbali wa kilomita mbili kulikuwa na kijiji. Ilibidi abiria wote wakubaliane kwenda kwenye mji huo kutafuta maji na chakula. Waliondoka na kuwaacha dereva konda na fundi wao, walifika kwenye mji ule ambao ulikuwa na nyumba nyingi za majani na za bati chache.

Walivamia kwenye mgahawa ulikuwa pale na kufanya wenyeji wa mji ule kufurahia ujio wao kwani walifanya biashara ambayo hawakuwahi kuifanya siku za nyuma. Kiza kiliwaingilia wakiwa kwenye mji ule. Kwa vile gari lilikuwa sehemu mbaya waliomba wakae pale hata kulala sehemu moja mpaka gari lao litakapopona.
Wanakijiji hawakuna na hiyana walitengeneza chakula kingine kingi kwa ajili ya usiku. Ulipofika usiku mkubwa walilala karibu na soko ili kuitafuta siku ya pili, wengi hawakulala walikuwa wakipiga stori kwa muda mrefu. Janette naye alikuwa na mwenyeji wao Ras ambaye alionyesha kusikitishwa na tatizo lililotokea kwa vile hesabu zake zilikuwa mpaka usiku unaingia wangekuwa tayari wamo ndani ya nchi ya Sudani Kusini.
“Usijali, siku zote safari hatua,” Janette alimtoa hofu.
“Ni kweli, lakini safari zangu huenda vizuri nashangaa hii.”
“Siku hazilingani mwanangu,” mama Janette naye alimtia moyo.
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu, watu wote walipitiwa usingizi na sehemu yote ilikuwa kimya.
Katikati ya usiku sauti ya vilio vya watu iliwashtua abiria wote waliokuwa wamejilaza pembeni ya soko. Wote walitaharuki baada ya kuamka na kuona nyumba za wenyeji wao zikiwaka moto.
“Mungu wangu nini kile?” Janette aliuliza kwa sauti.
“Ooh! Mungu wangu kijiji kimevamiwa,” alijibu Ras huku akiwa ameshika mikono kifuani kwa hofu.
“Na nani?” mama Janette aliuliza.
“Dah! Sikujua kama mji huu upo katika vita ya kidini.”
“Mmh! Tutapona kweli?” mama Janette aliuliza macho yakiwa yamemtoka pima kwa hofu.
Wakati huo kila mmoja aliyekuwa amelala pale alikuwa amejikunyata kwa hofu ya uhai wake. Moto nao uliendelea kuunguza nyumba zaidi na vilio vya uchungu vilitawala anga yote.
“Mmh! Inatakiwa tupambane hasa kwa vile jamaa wakifika wanaua kijiji kizima kwa vile wanaamini wote pale si dini yao.”
“Mama silaha yako unayo?”
“Ndiyo.”
“Sasa jamani tunatakiwa tukae mkao wa kupambana kwa vile eneo lote hatulijui, tungejua tukimbilie wapi. Tunaweza kukimbia kumbe tunawafuata waua….”
Janette kabla hajamalizia kauli yake lilionekana kundi kubwa la watu wakiwa na mapanga, marungu, pinde na mikuki likielekea sehemu waliyokuwa wamesimama wao.
“Kumekucha,” Janette alisema huku akitoa bastola yake.
Wakati baadhi ya abiria walianza kutawanyika ovyo, wale jamaa walianza kuwashambulia kwa mapanga abiria na kuwaua. Vilio vilitanda kila kona huku nyumba zingine zikibomolewa na kupigwa moto. Moyo wa Janette ulimwenda mbio kwani katika mapigano yote aliyoyafanya akiwa na jeshi la waasi, hakuwahi kuona vita nzito kama ile.
Kupona kwao aliona sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano, kwa vile damu ilizidi kumwagika na watu walizidi kufa wakikwemo abiria wenzake, Ras alipotaka kukimbia sehemu aliyokuwepo alikutana na rungu la kichwa lililompaleka chini. Janette na mama yake waliyaona mauti yapo mbele yao.
KILA sekunde moja ilikuwa mtihani mzito kwa Janette na mama yake baada ya kufanikiwa kuvuka salama Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo ndiyo iliyompa presha kubwa, anakijuta katika mtihani mkubwa wa kuyaokoa maisha yake baada ya wanakijiji kuvamiwa katika vita ya kidini.

Tags
Hadithi & Simulizi