HII ni historia ya kweli ya maisha yangu, kuna baadhi ya watu nakutana nao wananiuliza kama hii ni hadithi kama ambazo nimekuwa nikiandika magazetini. Nataka nisisitize kwamba hii ni historia ya kweli kabisa ya maisha yangu, najaribu kuyapitia maisha yangu ya nyuma na kuwaandikia watu kule nilikopitia.
Lengo langu ni nini? Kumtia moyo mtu aliyevunjika moyo na kumfanya aamini inawezekana kufanikiwa hata kama unatoka familia masikini. Nayasema haya kwa sababu wako watu leo hii wamekata tamaa kabisa na kuamini kwamba watu fulani wanaweza kufanya vizuri maishani na si wao, uongo mkubwa na mbinu ya shetani kuwafanya watu waendelee kuteseka.
Yeyote anayesoma historia yangu ni lazima hata kama yuko katika hali ngumu kiasi gani, aamini kwamba inawezekana, kama iliwezekana kwangu inashindikanaje kwa mtu mwingine? Inuka hapo ulipo, amini akili yako, fanya jambo jema hata kama ni dogo kiasi gani, ukilifanya kwa muda mrefu hatimaye jambo kubwa litakutokea, huu kwangu ni ukweli uliothibitishwa na mimi mwenyewe.
Lengo si kujitapa bali kuwaonesha watu jinsi Mungu anavyoweza kumbariki mtu na ninajua kutoka ndani ya moyo wangu ya kwamba Mungu alininyanyua kwa kusudi moja tu; yeyote aliyekata tamaa atakaponiangalia mimi apate tumaini na kuamini kwamba kumbe inawezekana.
Nimeishia kueleza jinsi kesi yangu na Ruge ilivyonikosesha raha mpaka nikaenda kuomba msaada kwa Jakaya Mrisho Kikwete. ENDELEA...
Nimeishia kueleza jinsi kesi yangu na Ruge ilivyonikosesha raha mpaka nikaenda kuomba msaada kwa Jakaya Mrisho Kikwete. ENDELEA...
Baada ya mazungumzo yangu mimi na mheshimiwa kumalizika, mwanaume niliondoka na kurejea nyumbani, kazi yote nikiwa nimemuachia yeye ambaye aliahidi kuwatafuta jamaa na kuzungumza nao. Sikumweleza mtu yeyote, niliamua kukaa kimya na kusubiri, nikifanya kila kitu siri.
Wiki chache baadaye, suala langu na Clouds FM lilikwisha bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea, kichwani mwangu nikijiuliza maswali mengi bila majibu lakini wakati mwingine niliamini kwamba huenda Mheshimiwa Mrisho Kikwete alifanya kama alivyoniambia.
Niliamua kuandika ujumbe mfupi wa maneno kwa mheshimiwa kama shukrani zangu kwake lakini hakujibu kitu chochote, alikaa kimya tu.
Maisha yakaendelea, kazi nazo zikaendelea huku tukiendelea kupambana na maadui zetu, naomba niseme wazi hapa ushindani ulikuwa mkali na maadui nao wakazidi kuongezeka zaidi. Lakini nikamshukuru Mungu na kumwomba aendelee kunipa nguvu za kupigana.
Hivyo ndivyo ilivyotokea, hatimaye kesi yangu na Clouds FM ikawa imekwisha kimyakimya na kunipa tena nafasi nyingine ya kuendelea kusonga mbele kukimbiza maisha Mungu akiwa upande wetu.
Miezi mitatu baadaye Clouds FM waliandaa tamasha kubwa la Mr Nice (mwanamuziki Nice Lucas Mkenda) lililofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar, wakati huo bado Dudubaya akiwa ni rafiki mkubwa wa Clouds FM.
Miezi mitatu baadaye Clouds FM waliandaa tamasha kubwa la Mr Nice (mwanamuziki Nice Lucas Mkenda) lililofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar, wakati huo bado Dudubaya akiwa ni rafiki mkubwa wa Clouds FM.
Mr. Nice akiwa ndiye mtumbuizaji, alipanda jukwaani na kuanza kuimba nyimbo zake, watu wote wakimshangilia na kumpigia makofi, ni wakati akiwa jukwaani akaanza kumtukana Dudubaya jambo ambalo Dudubaya hakukubaliana nalo, kijana akalivamia jukwaa na kuanza kushusha kipondo kibaya na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na kuhatarisha usalama wa wahudhuriaji.
Pamoja na kwamba alikuwa rafiki mkubwa wa Clouds FM lakini kwa jambo lililokuwa limetokea liliwakera sana watu hawa, wakamfungulia mashitaka na Dudubaya akatupwa mahabusu.
Moyoni mwangu nikajikuta nikisema acha wamkomeshe, yeye si aliwaona ni bora kuliko mimi kijana mwenzake wa Mwanza waliokuwa marafiki zake sasa walikuwa wamemgeuka na kuwa maadui wakubwa.
Pamoja na kwamba alikuwa rafiki mkubwa wa Clouds FM lakini kwa jambo lililokuwa limetokea liliwakera sana watu hawa, wakamfungulia mashitaka na Dudubaya akatupwa mahabusu.
Moyoni mwangu nikajikuta nikisema acha wamkomeshe, yeye si aliwaona ni bora kuliko mimi kijana mwenzake wa Mwanza waliokuwa marafiki zake sasa walikuwa wamemgeuka na kuwa maadui wakubwa.
Dudubaya aliendelea kukaa mahabusu akiwa hana mtu yeyote yule wa kumsaidia wale waliokuwa marafiki sasa walikuwa wabaya, hawakupenda hata kumsikia kwa jambo lolote lile. Nikiendelea na kazi zangu pamoja na timu yangu nilipata simu nyingi sana kutoka Mwanza, wengi wakiomba nimsaidie Dudubaya lakini mimi nilikataa kabisa.
Mimi na timu yangu tuliendelea na kazi zetu, tukizunguka huku na kule kutafuta habari kisha kuzichapisha na magazeti yetu yakaongezeka umaarufu, watu wakayakubali zaidi jambo ambalo mpaka leo ninapoandika kumbukumbu hizi ninajivunia na kumshukuru sana Mungu wangu.
Siku moja nikiwa nimeketi ofisini kwangu, nikiyatafakari maisha, nilipokea simu kutoka kwa mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwangu kwamba alikuwa ni mtu wa Mwanza na alitaka kuzungumza na mimi. Moja kwa moja nilimkubalia, baada ya kujitambulisha alianza kunieleza wazi kwamba alikuwa ni shabiki mkubwa wa Dudubaya na lengo la simu hiyo ilikuwa ni kumwombea msamaha amsamehe na kumsaidia.
Ni kweli maneno ya mwanamke huyo yaliupenya moyo wangu, nikajikuta nikilegeza kamba na kuingiwa na huruma bila kuficha nilimkubalia na kumuahidi kufanya kila nilichoweza kumsaidia Dudubaya pamoja na kwamba alinitenda ubaya.
Naomba nikiri hapa kwamba mimi hupenda kutumia sheria moja kwamba ukitaka kumpunguza adui asiwe adui ni kumtendea mema. Hivyo ndivyo nilivyofanya, huruma ikanijaa, nikaanza mchakato wa kufanya jambo fulani kumtoa Dudubaya mahabusu.
Nilianza mikakati ya siri Clouds FM wakiwa hawajui kitu chochote kinaendelea, hatimaye Dudubaya akatoka na alipouliza ni nani alikuwa amefanya jambo hilo alielezwa moja kwa moja kwamba ilikuwa ni mimi, alishangaa, hakuwahi kufikiria kwamba ningeweza kumlipa mema kwa mabaya aliyonitendea.
Baada ya kutoka mahabusu, Dudubaya aliamua kunitafuta ili tuongee lakini sikuwa tayari kufanya hivyo, kwa muda aliendelea kufanya hivyo bila mafanikio, mwisho tukaongea kwa simu. Aliongea vitu vingi na kutubu makosa yake yote akikiri kwamba alikuwa ametumiwa ili kunichafua.
Nikawa nimemsamehe Dudubaya.
Kazi ikawa moja tu, kuchapa kazi kwa bidii mimi pamoja na timu yangu kwa nguvu kubwa mno, mambo yakawa safi. Ninamshukuru Mungu kwa hili. Tukalazimika kuhama Posta na kwenda Kariakoo kwenye jengo la vioo lililokuwa na nafasi ili kuendelea na majukumu.
Kazi ikawa moja tu, kuchapa kazi kwa bidii mimi pamoja na timu yangu kwa nguvu kubwa mno, mambo yakawa safi. Ninamshukuru Mungu kwa hili. Tukalazimika kuhama Posta na kwenda Kariakoo kwenye jengo la vioo lililokuwa na nafasi ili kuendelea na majukumu.
Mpaka wakati huo, tayari magazeti yetu yalishaongezeka. Sasa tulikuwa na Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Amani na Championi (gazeti la michezo), nakumbuka vizuri mhariri wake wa kwanza aliitwa Denis Msaki (ameshawahi kuwa Mhariri Mkuu Mwananchi na hivi sasa ni Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mtanzania) akiwa na timu yake, Fred Majaliwa, Charles Mganga, Athanas Kazige (Babu) na wengine wengi.
Tuliingia asubuhi na kutoka usiku mimi na timu yangu tukifanya kazi kwa bidii kwelikweli, hatukuwa na muda wa kupoteza nikiogopa kurejea tena katika umasikini, hivyo nilichagua timu sahihi ya watu waliopenda kufanya kazi na kujituma bila kusukumwa, kwani kwa jinsi Watanzania tulivyo wengi ili wafanye kazi lazima wasukumwe.
Nilikuwa tayari kufanya kazi na wale walioipenda na si wale waliotaka fedha, hivyo niliangalia zaidi maslahi ya kampuni kuliko mtu binafsi, aliyeleta mchezo sikucheka naye, huyo aliondoka na aliyetaka kazi basi alibaki. Hapa nikaanza kupoteza watu wakiondoka na wengine wakiingia. Ofisi ikawa kubwa zaidi, tukachukua ghorofa ya nne na ya pili hapohapo Kariakoo, duka la vioo.
Wakati sisi tukiendelea na kazi ghorofa ya pili tu kutoka kwetu alikuwepo mtu mmoja aliyeitwa Mashaka Matongo ‘Abiola’, huyu alikuwa ni wakala wa magazeti, akichukua magazeti kwetu na kwa watu wengine kisha kuuza, jambo hili likampa mafanikio makubwa sana. Ni hapo ndipo alipoamua naye kuingia kwenye uchapishaji wa magazeti, akaanzisha yake yaliyoitwa, Fukuto, Hamu, Risasi, Sakata na Amani.
Niliamini katika jambo moja, ili ufanikiwe ni lazima uwe na ushindani hivyo nikafurahi kupata mshindani mwenzangu na rafiki yangu mkubwa, mambo yakaendelea na kufanya biashara vizuri tu. Huku tukiendelea kukua kwa kasi ya ajabu.
Siku moja nikiwa ofisini kwangu timu yangu ikiendelea na kazi, nikiamini kwamba sasa nilikuwa nimepata timu sahihi bila kufahamu upande mwingine wa shilingi, nilipata mshtuko mkubwa sana vijana wangu, tegemeo langu, Dismas Lyassa, Makongoro Oging’ na wengine wengi ambao siwakumbuki vizuri waliandika barua za kuacha kazi na nilipochunguza vizuri, niligundua walikuwa wamehamia ghorofa ya pili tu kwa Mashaka Matongo au Abiola kama alivyojulikana na wengi.
Sifichi, jambo hili lilinivuruga tena akili yangu nikarudi nyuma na kukumbuka yaliyopita lakini nikamwomba Mungu wangu anisaidie ili nishinde kwani ilikuwa ni lazima, nikatafuta watu wengine, wakapatikana na kazi ikaendelea lakini bado nikiwa nimechanganyikiwa.
Charles Mganga akashika gazeti na kuwa mhariri mkuu na kazi zikaendelea.
Jambo moja niseme hapa ni kwamba tatizo kubwa la vyombo vya habari hapa nchini kwetu ni vingi lakini waandishi wa habari ni wachache.
Charles Mganga akashika gazeti na kuwa mhariri mkuu na kazi zikaendelea.
Jambo moja niseme hapa ni kwamba tatizo kubwa la vyombo vya habari hapa nchini kwetu ni vingi lakini waandishi wa habari ni wachache.
Niliamini kwamba pengine Mashaka aliyaona mafanikio yangu na kuamini katika jambo hilo kwamba pengine akiwachukua wafanyakazi wangu basi naye angefanikiwa kama ilivyotokea kwangu.
Pamoja na yote nikaendelea mbele zaidi, nakala nyingi zikaongezeka, mauzo yakawa makubwa kupindukia, nikajikuta nikitamka ndani ya moyo wangu kwamba “Pengine Mungu alikuwa nalo kusudi juu ya jambo hili,” nikamshukuru.
Pamoja na yote nikaendelea mbele zaidi, nakala nyingi zikaongezeka, mauzo yakawa makubwa kupindukia, nikajikuta nikitamka ndani ya moyo wangu kwamba “Pengine Mungu alikuwa nalo kusudi juu ya jambo hili,” nikamshukuru.
Tags
Hadithi & Simulizi