kisha nikaona anatoa notibuku yake na kuandika kitu.
Sikuweza kujua kama yule dereva aliyekuwa akiongea naye ndiye aliyempakia mke wake usiku wa siku ile na kama ndiyo alikuwa akimueleza alikompeleka Nikole, yaani nyumbani kwangu.

Wala sikuweza kujua alichokiandika kwenye notibuku yake kama ni namba ya nyumba yangu au ni kitu gani. Ilimradi niliona magoti yakininyong’onyea kama niliyepatwa na presha ya ghafla.
SASA ENDELEA…
SASA ENDELEA…
Wakati magoti yananicheza na presha yangu ikionesha kunipanda, nilimuona Machibya akiagana na yule dereva na kuondoka.
Sasa nikabaki na swali, kama yule mtu alikuwa ndiye dereva aliyempakia Nikole kwa nini hakuondoka naye ili akamuoneshe nyumba yangu.
Lakini jibu likanijia mara moja kwamba huenda dereva huyo alimtajia Machibya mtaa na namba ya nyumba, hivyo Machibya aliamua kwenda mwenyewe.
Nikajiambia kama Machibya ameamua hivyo, atakapobisha mlango wa nyumba yangu hatapata jibu kwani nikimuona sitasogea pale nyumbani na mwisho wake atakata tamaa na kuondoka.
Wazo lingine likanijia kwamba atakapoondoka nyumbani kwangu baada ya kutopata jibu, anaweza kwenda kuripoti polisi hivyo kurudi tena na polisi.

Sikuhofia polisi kunitafuta na kunihoji, nilihofia ile maiti ya Nikole kuonekana nyumbani kwangu hasa kwa vile ilishaanza kutoa harufu.
Sikutaka kuwaza mengi, nikaona nimfuate Machibya nione alikuwa anakwenda wapi.

Nilimfuata nyuma nyuma hadi nyumbani kwake, akaingia ndani. Niliketi kwenye baraza ya nyumba moja iliyokuwa mbali kidogo na nyumba ya Machibya. Lengo langu lilikuwa kujua kama atatoka.
Nilikaa hapo kwa zaidi ya saa mbili. Machibya hakutoka.

Nikawaza kwamba kama Machibya alitajiwa mtaa na namba ya nyumba yangu, angelikwishakwenda kuniulizia. Au kama alikuwa na nia ya kwenda polisi pia angelikwishakwenda.
Kuendelea kwake kukaa ndani kwa muda wote huo kulinifanya nione kuwa hakumpata yule dereva wa teksi aliyempakia mke wake. Dereva aliyeongea naye alikuwa mwingine.

Niliporidhika kuwa tishio la kufuatwa nyumbani muda ule halikuwepo, niliondoka nikarudi nyumbani.
Harufu ilikuwa imeenea nyumba nzima kiasi kwamba mtu akiingia angejua kwamba kulikuwa na kitu kinachonuka. Harufu ile ilinikera sana.

Nikaingia chumbani kwangu na kuchukua kopo la dawa ya mbu na chupa ya pafyumu ya mke wangu. Nikaenda navyo kule stoo.
Niliupulizia ule mwili dawa ya mbu ili kupoteza ile harufu kisha nikaupulizia pafyumu.
Nilitoka ukumbini nikaendelea kupulizia dawa ya mbu na pafyumu. Nilipulizia hadi sebuleni. Nilipohisi kuwa hewa ilikuwa nzuri kidogo nilirudi chumbani.

Nilitoa simu na kumpigia mke wangu kwa vile nilimuahidi kuwa ningempigia nikifika nyumbani.
“Ndiyo unafika sasa nyumbani?” Mke wangu akaniuliza mara tu alipofika nyumbani.
“Nilienda kula chakula, sasa ndiyo nimerudi nyumbani,” nikamdanganya ili nipate salama.
“Hata hivyo, umepitisha muda mwingi. Kama ni kula chakula, nusu saa si inakutosha?”

“Ni kweli mke wangu, pia nilikuwa na mazungumzo ya kikazi na watu fulani,” nikaropoka.
“Mbona hueleweki, ulikuwa unakula au ulikuwa na mazungumzo?”
Nikaguna kisha nikamjibu: “Vyote viwili.”

“Nikwambie ukweli mume wangu, baada ya mimi kuondoka hapo nyumbani umebadilika kidogo.”
“Hapana mke wangu, sijabadilika. Nimetingwa tu na majukumu. Nakupenda sana. Usinifikirie vibaya.”
“Hata kama umetingwa na majukumu usinisahau mke wako.”
“Ni kweli. Basi tuyaache hayo. Niambie kuhusu hali yako kwa sasa.”
“Bado ninaumwa lakini si sana.”

“Ungepelekwa hospitali kabisa, ukae kulekule.”
“Naona bado kidogo, nitakaa sana kabla ya kujifungua.”
“Unataka ukae hadi uchungu ukuzidie ndiyo upelekwe?”

“Basi ngoja nimwambie mdogo wangu aniitie teksi.”
“Nitakupigia tena baadaye kidogo.”
“Simu yangu anaweza kuwa nayo dada yangu, ukipiga atakueleza maendeleo.”
“Sawa mke wangu.”

Nikakata simu. Kusema kweli sikuwa na furaha ya kuzungumza na mke wangu. Kila tulipoongea nilitaka tumalize haraka ili niendelee kutafakari matatizo yaliyonikabili.
Wakati nakata simu, simu yangu ikaita tena. Nikaona namba ya Asma.
“Asma anataka kuniambia nini tena!” Nikajiuliza kimoyomoyo huku nikiipokea simu hiyo kwa haraka.
“Asma! Vipi?”

“Poa tu, umeshafika nyumbani?”
“Hapa niko nyumbani kwangu.”
“Machibya hakufika?”
“Afuate nini?”
“Hapa niko nyumbani kwangu.”
“Machibya hakufika?”
“Afuate nini?”
“Kumuulizia mke wake.”
“Hawezi kufika kwangu, mimi sina uhusiano naye wa kiasi hicho.”
“Aliponiambia anakwenda kuulizia namba ya ile teksi nilidhani ameshaipata.”

“Kwani akiipata ndiyo ataletwa kwangu?”
“Huenda Nikole alikuja kwako lakini wewe unakataa tu.”
Wakati Asma ananiambia hivyo nilisikia mlango wa nje unabishwa. Nikashituka kidogo.
Ni nani anayebisha mlango?Nikawaza isije kuwa ni Machibya, ndiyo amekuja na polisi!

Tags
Hadithi & Simulizi