Wazambia wanukia Yanga SC



USAJILI unazidi kushika kasi Ligi Kuu Bara ambapo sasa Yanga SC wameamua kuzigeukia klabu za Zambia kwa ajili ya kufanya usajili wa baadhi ya wachezaji wanaowataka.
Imeelezwa kuwa Yanga wanatafuta straika mmoja matata kwa ajili ya msimu ujao, hivyo tayari kuna harakati zimeanza kufanyika na mawasiliano yakiendelea kwa ajili ya kunyakua straika mmoja kutoka timu ya Nkana Red Devils aliyowahi kucheza straika wa zamani wa Simba, Felix Sunzu.
Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga kimesema kwamba tayari kuna wachezaji kutoka kwenye ligi kuu ya nchi hiyo wameshaanza kufuatiliwa kwa karibu zaidi kuona kama uwezo wao unaweza kuwapeleka Jangwani.
Kiliongeza kuwa Yanga wapo tayari kuwatumia tiketi wachezaji hao muda wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kuja kumalizana nao na kama ikishindikana basi viongozi watalazimika kufunga safari na kuwafuata ili azma yao itimie.
“Kuna kikao kiliwekwa juzi kwa ajili ya usajili mpya lakini ikaonekana pia Zambia kunaweza kukawa na suluhisho la straika, hivyo tayari kuna mawasiliano yanaendelea juu ya kuangalia uwezekano wa kunasa straika mzuri.
“Tayari kuna mshambuliaji anacheza Nkana ndiyo wameanza kumtolea macho huyo kwanza wakati wanaendelea na uchunguzi kwa wengine, iwapo watapata kifaa, Yanga wapo tayari kutuma tiketi ili wafanikishe azma yao au ikiwezekana wamfuate wao,” kilisema chanzo hicho.
Championi Jumatatu lilipozungumza na Baraka Kizuguto ambaye ni Ofisa Habari wa Yanga kuhusiana na hilo alisema 

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post