Goli la Pique la dakika za majeruhi laipa Hispania ushindi Getty

humph the GREAT






Goli la Pique la dakika za majeruhi laipa Hispania ushindi


La Roja hawajaruhusu goli kwa dakika 600 walizocheza kwenye michuano ya Ulaya, timu pekee yenye mwendo mzuri katika michuano hiyo tangu Euro 2012
Hispania imeanza vizuri kampeni za kutetea taji lake katika michuano ya Euro 2016 kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuichapa Jamhuri ya Czech.
Bao la kichwa la dakika za lala salama lilofungwa na mlinzi Gerard Pique akiunganisha krosi ya Andres Iniesta hatimaye lilipeleka faraja kwa wahispania kufuatia upinzani mkali walioupata kutoka kwa wapinzani wao.
Alvaro Morata, Jordi Alba na David Silva juhudi zao ziligonga mwamba huku mabingwa hao watetezi wa taji la Ulaya wakishindwa kufunga katika dakika za mapema na kusubiri hadi dakika za jioni.
Hispania pia ilinurusika kuchapwa bao pale Cesc Fabregas alipookoa mpira kwenye mstari wa goli uliopigwa na Theodor Gebre Selassie
Vladimir Darida alipata nafasi ya kuisawazishia Jamhuri ya Czech lakini mlinda mlango wa Hispania David de Gea alikuwa vizuri langoni licha ya tuhuma zinazomkabili.
Previous Post Next Post