humph the GREAT
Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, ameliomba jeshi hilo kumpa kitengo cha masoko ili aweze kulitangaza na kuliunganisha na wananchi, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maboresho ndani ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.
“Nimekuwa
mtumishi ndani ya polisi kwa miaka 40, ninaweza kutumika hata na Shule
ya Polisi Moshi kufundisha na hata kutoa uzoefu wangu ambao utalisaidia
jeshi katika kukabili uhalifu, kama mnavyoniona ninazo nguvu za kutosha
na ninalipenda Jeshi la Polisi,” alisema.

Kova alitoa ombi hilo jana mjini Moshi katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Shule ya Polisi Moshi (MPA).
Alisema jeshi hilo linaelekea kuzindua
mpango wake wa matokeo makubwa sasa (BRN) ,ambao unahitaji msukumo wa
jamii katika kusaidia kukabiliana na uhalifu wa aina mbalimbali ukiwamo
wa mtandaoni na dawa ya kulevya.
Kova alisema kutokana na utumishi wake
wa zaidi ya miaka 40 kwa kushirikiana na wastaafu wengine, wanaweza
kusaidia na kuwa kiunganishi baina ya polisi na raia kama njia bora ya
kukabiliana na uhalifu kwa kutumia kitengo cha masoko.
“Nimekuwa
mtumishi ndani ya polisi kwa miaka 40, ninaweza kutumika hata na Shule
ya Polisi Moshi kufundisha na hata kutoa uzoefu wangu ambao utalisaidia
jeshi katika kukabili uhalifu, kama mnavyoniona ninazo nguvu za kutosha
na ninalipenda Jeshi la Polisi,” alisema.
Katika hatua nyingine, Kamishna Kova
aliiomba serikali kuliboresha zaidi jeshi la polisi kwa vifaa, mbinu na
teknolojia za hali ya juu ili kukabiliana na matukio ya uhalifu wa aina
mbalimbali unaokuwa kulingana na ukuaji wa teknolojia duniani.
Tags
HABARI