humph the GREAT.
MWANASOKA wa Ureno anayekipiga kwenye klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo, amekula bata kwenye fukwe za Ibiza zilizopo nchini Hispania akiwa na mama yake mzazi aitwaye Dolores mwenye umri wa miaka 61, na mtoto wake wa kiume Cristiano Jr.
Katika mtandao wa kijamii wa Instagram, hivi majuzi aliandika kuhusu “kusafiri na familia.”
Ameungana na familia yake zikiwa zimepita siku chache tu tangu aiongoze nchi yake ya Ureno kushinda kombe katika mashindano ya soka ya Ulaya (Euro) kwa ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya Ufaransa katika fainali. Ronaldo alitolewa uwanjani dakika ya 25 ya mchezo baada ya kuumizwa na mchezaji wa Ufaransa, Dmitri Payet.
Ronaldo, 31, anayeuguza majeraha yake ameamua kupumzika katika fukwe hizo maarufu duniani.
Mchezaji huyo bora wa dunia mara tatu alitumia muda mfupi nchini Ureno kusheherekea ushindi huo na wachezaji wenzake kabla ya kuondoka na familia yake kuelekea kwenye fukwe hizo.
0 Comments