humph the GREAT
MKONGWE wa nyimbo za Uswahilini, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu’ anatarajiwa kupewa heshima ya ufalme rasmi Agosti 13, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Akizungumza na Showbiz Xtra, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa usiku huo utakuwa maalum kwa Msaga Sumu aliyeonesha uwezo mkubwa kuufikisha mbali muziki wa uswahilini.
“Msaga Sumu ni mwanamuziki wa kipekee ambaye hakuchoka kuufikisha muziki wa uswahilini hapa ulipo, aliimba Singeli, Mchiriku, Segere, Ladha na nyingine zote. Hadi sasa ana zaidi ya nyimbo 15 ambazo ataziimba usiku huo,” alisema Mbizo.
Usiku huo pia, Msaga Sumu atasindikizwa na wakali kibao kama vile Segere, Juma Nature, Snura, Shoro Mwamba, MC Sudy na wengine kibao

Tags
Burudani