Kituo cha Polisi Chavamiwa Kenya

humph the GREAT



MAAFISA wa Polisi wapatao 6 wanahofiwa kufariki dunia baada mtu mwenye silaha anayedaiwa kuwa mwanamgambo wa Al-Shabaab kukishambulia Kituo cha Polisi cha Kapenguria, kilichopo Kaskazini Magharibi mwa Kenya mapema leo.

Mtu huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho wakati akiwa kwenye harakati za kutaka kumuokoa mshukiwa aliyekuwa amekamatwa na kupelekwa kituoni hapo akishukiwa kuhusika katika ugaidi, gazeti la Daily Nation limeripoti.

Imeelezwa kuwa, Askari wa Jeshi la Kenya (KDF) wameshafika eneo la tukio na inadaiwa kuwa, Mkuu wa Polisi wa kituo hicho, Vitalis Ochido anadaiwa kujeruhiwa wakati wa makabiliano na mpiganaji huyo kwa kufyatuliana risasi.

Aidha, Tovuti ya habari ya Capital FM imemnukuu Mkuu wa Polisi, Joseph Boinnet akisema polisi zaidi wameelekea kwenye eneo tukio ili kwenda kudhibiti hali hiyo.

“Mshukiwa wa ugaidi aliyekuwa anazuiliwa alitwaa bunduki na kuanza kuvyatua risasi,” Bw Boinnet amenukuliwa. “Kituo hicho sasa kimezingirwa na juhudi za kukabiliana naye (mshambuliaji) zinaendelea.” Boinnnet alisema.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post