humph the GREAT

Ambwene Yessaya ‘AY’
Mwana FA
Barnaba
Linex
Msami
MC Pilipili
Ben Pol
Ambwene Yessaya ‘AY’
WAKALI kibao wanaokimbiza kunako Muziki wa Bongo Fleva wakiongozwa na AY, MwanaFA, Ben Pol, Barnaba wanatarajiwa kuangusha bonge la shoo lililopewa jina la Dawati Concert leo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.
Akizungumza na Risasi BMM mratibu wa shoo hiyo iliyopewa jina maalum la Dawati Concert, Arthur Samuel alisema kuwa, shoo hiyo imekuja ikiwa suala la uchangiaji wa madawati kwa shule mbalimbali nchini likishika hatamu karibu kila sekta na lengo lao ni kukusanya fedha za kuchangia madawati ili wanafunzi wapate mazingira bora ya kusomea.
“Kama mtakumbuka hili suala la kuchangia madawati ni moja ya kauli mbiu za Rais Dk. John Pombe Magufuli. Niwaombe mashabiki wa burudani hasa muziki huu wa Bongo Fleva wajitokeze kwa wingi kujumuika nasi,” alisema Arthur.
Arthur aliongeza kuwa fedha zitakazokusanywa katika ‘event’ hiyo itakayoanza saa 12 jioni, zote zitaingizwa katika mradi huo na kwamba wasanii maarufu walioguswa na suala zima la elimu wanajitokeza kuperform bure na kukonga nyoyo za mashsabiki
“Utakapohudhuria shoo hii ya kiingilio cha Sh. 5,000 tu, utakuwa umeingia moja kwa moja katika kuchangia fedha za madawati kwa watoto wetu, wadogo, ndugu na jamaa zetu mbalimbali ili wapate elimu nzuri.
“Wasanii watakuwepo kibao kama, Ambwene Yesaya ‘AY’, Mwana FA, Barnaba, Linex, Msami a.k.a Mabawa, Glorious Worship Team, Galatone a.k.a Mzee wa Samaki, mchekeshaji maarufu wa majukwaani, MC Pilipili, Ben Pol na wengine wengi na wote hawa watafanya shoo ya kiingilio cha shilingi 5,000 tu ambapo hawatachukua chochote katika fedha itakayopatikana, kwa maana kwamba yote itakusanywa kununulia madawati na kuyapeleka sehemu husika
“Haya madawati hayatalenga shule za Dar tu, tutaangalia maeneo mbalimbali Tanzania nzima, kuwa wapi panapohitajika huduma hii kwa haraka zaidi ndipo tutakapopafikia mapema zaidi. Kwa kupitia shoo hii tunaamini watu wa burudani wamepata sehemu ya kuwasilisha michango yao katika elimu,” anamaliza Arthur.
Tags
Burudani