RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi juzi amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA), baada ya kupata kura 21 kati ya 22.
Katika uchaguzi huo uliofanyika ukumbi
wa mikutano wa hoteli ya Optima, Bananzi, wilayani Misenyi, Salum Chama
alitetea nafasi yake ya Katibu Mkuu KRFA kwa kupata kura zote 22,
wakati Pelegrinius Rutahyugwa alitetea Ujumbe Mkutano Mkuu waTFF kwa
kupata kura zote pia 22.
Naye Didas Zimbihile alitetea nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu Klabu wa TFF kwa kukusanya kura zote 22.
Malinzi amekuwa Mwenyekiti wa KRFA tangu Machi 17, mwaka 2012 na katika kipindi chake cha kuwa madarakani amesaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha hamasa ya soka kimkoa na sasa mpira wa miguu unachezwa Kagera nzima tena.
Aidha, Malinzi amesaidia ukarabati wa Uwanja wa Kaitaba ambaao sasa una mwonekano mzuri ukiwa unapambwa na nyasi bandia.

0 Comments