humph the GREAT
Mchezaji
wa Judo kutoka Misri, Islam El Shehaby amerudishwa nyumbani kutoka
katika michezo ya Olimpiki baada ya kukataa kusalimiana kwa mkono na
mpinzani wake Sasson kutoka Israel baada ya pigano lao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34
alipewa adhabu hiyo na kamati ya michezo ya Olimpiki baada ya kupoteza
katika raundi ya kwanza siku ya Ijumaa.
Kamati ya Olimpiki imesema kuwa tabia yake inaenda kinyume na sera ya urafiki iliopo katika maadili ya michezo hiyo.
El Shehaby baadaye alizomewa na
mashabiki waliokuwa wamejaa katika ukumbi wa mchezo huo na alitakiwa
kurudi katika ukumbi huo ili kutoa heshima kwa mpinzani wake kwa kuwa ni
kinyume na sheria za mchezo huo.
Sasson hata hivyo alibaini kwamba makocha wake walimuonya kwamba El Shehaby huenda asimsalimie kwa kushikana mikono.
Inadaiwa kwamba raia huyo wa Misri
alikuwa ameshinikizwa na baadhi ya mashabiki wake kutoka nyumbani
kutoshiriki katika pigano hilo.
Tags
Michezo na burudani