humph the GREAT
 
 
GABRIEL Gerald jana aliwatoa kimasomaso Watanzania baada ya kuwapiku Wakenya na washiriki wengine na kumaliza wa kwanza katika mashindano ya mbio za kimataifa za Kili FM Marathon zilizofanyika mjini Moshi.
Kwa muda mrefu Wakenya wamekuwa wakishika nafasi za kwanza katika mbio mbalimbali zinazoandaliwa nchini na kuondoka na zawadi kibao zikiwemo za fedha na medali, lakini jana ilikuwa tofauti pale Gerald alipomaliza wa kwanza kwa kutumia saa 1:05.05.
Kwa ushindi huo, mwanariadha huyo wa Tanzania aliondoka na kitita cha Sh 700,000 katika mbio hizo za kwanza huku Mkenya Kennedy Kimathi akimaliza wa pili kwa kutumia saa 1:05.29 wakati nafasi ya tatu ilikwenda kwa mwanariadha mzoefu wa Tanzania, Dickson Marwa aliyetumia saa 1:05.34.
Washindi wa pili na wa tatu kila mmoja aliondoka na zawadi ya Sh 500,000 wakati nafasi ya nne ilikwenda kwa mwanariadha wa Kenya, David Kilimo aliyetumia saa 1:06.02 wakati watano ni Mtanzania, Augustino Sule aliyetumia saa 1:06.17.
Kwa upande wa wanawake nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Mkenya Nancy Kiprop aliyetumia saa 1:15.00, nafasi ya pili ikitwaliwa na Mtanzania Magdalena Crispin kutoka Ausha aliyetumia saa 1:15.03 akifuatiwa na mwenzake Failuna Abdi pia wa Arusha saa 1:16.0 huku nafasi ya nne ikichukuliwa na Anelina Tsere 1:16.36 wakati nafasi ya tano ikaenda kwa Ladis Chepoi kutoka Kenya saa 1:17.0.
Kwa upande wa mbio za watoto Km 2.5 wavulana, mshindi aliibuka Rashid Naasi wa Police Line Moshi aliyetumia dakika 9:35, wa pili Japhari Abdul wa Pasua 9:43 wa tatu Loloo Yusuph 10:10:35 kutoka Amani huku wa nne akiwa ni Nickson Patrick 10:45 wakati wa tano akiibuka ni Mathayo Jiange dakika 10:54 wote kutoka Amani.
Kilometa 2.5 wasichana mshindi aliibuka Raphia Twalib kutoka Kikavu dakika 12:03, wa pili Getruda Talalai 12:12 wa Amani, wa tatu Hadija Alpha wa Majengo 12:17 huku wan ne akiibuka Lulu Shaba wa Mbuyuni 12:22 wakati nafasi tano ilienda kwa Grace Gastone kutoka Mwereni dakika 12:30.
Tags
Michezo na burudani