Bushoke: Watu wengi wananiomba nifanye wimbo na Christian Bella

humph the GREAT
Hebu fikiria Dunia Njia na Usilie vikiunganishwa na kuwa wimbo mmoja itakuaje?

Au Bushoke na Christian Bella wakiingia studio kufanya wimbo wa pamoja! Hicho ni kitu ambacho mashabiki wengi wanakitamani.

Akiongea na mtangazaji wa ABM Radio ya Dodoma, Dj Rodger, Bushoke amesema amekuwa akiambiwa na watu wengi afanye wimbo na Bella na kwamba mpango huo upo.

Bushoke amedai kuwa mashabiki wanaamini kuwa collabo yake na Bella itakuwa tofauti na itafanya vizuri.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post