Staa wa Nigeria Chinedu Ikedieze (Aki) aisifia ‘Salome’ ya Diamond ‘I am a big fan’

humph the GREAT
 Salome ya Diamond Platnumz inaelekea kumshangaza staa huyo kwa mafanikio makubwa inayoendelea kuyakusanya.

Baada ya video yake kuvutia views milioni 1 ndani ya siku mbili tu tangu itoke, wimbo huyo umeyagusa masikio ya mtu maarufu kwenye filamu za Nigeria, Chinedu Ikedieze anayejulikana zaidi kama Aki kwenye filamu zake.

Akicomment kwenye post ya Diamond Instagram, Ikedieze amesema kuwa haelewi kinachoimbwa kwenye wimbo huo lakini ameupenda na kwamba ni shabiki wake mkubwa.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post