Hii ndo Scene iliyomtoa machozi Diamond platnum kwenye wimbo wa UTANIPENDA

humph the GREAT
Diamond Platnumz aliamua kuitumia familia nzima kwenye video ya wimbo wake mpya, Utanipenda!
Mchumba wake Zari, mwanae Tiffah, mama yake Sandra na mameneja wake Babu Tale na Said Fella wameonekana.
Hata hivyo scene ya mama yake inayomuonesha akienda kwa Jakaya Kikwete na kufukuzwa na pia kwa Said Fella na kufukuzwa pia ilimliza Diamond.
12224632_1624698111126002_1129176434_n
“Wakati hii scene inashutiwa sikuweza kabisa kukaa karibu, ijapokuwa ilikuwa ni uigizaji ila nikajikuta najiskia vibaya alivyokuwa anafukuzwa na kuendelea kubembeleza. Hata siku ya kwanza kuiona hii video mara ya kwanza na pili machozi yalinitoka,” ameandika Diamond kwenye Instagram.
“Pia ilichukua muda sana kuizoea hicho kipande maana ilikuwa kila nikijikaza na kuchkulia ni maigizo ila najikuta mood inabadilika. Ooh mama yangu ntakulipa mimi.”

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post