humph the GREAT
Kuna mambo mengi sana ambayo bila msaada wa mama yake mzazi, hivi leo
kusingekuwa kuna jina linalowakilisha Bongo huko ugaibuni kama Diamond
platnumz, tukio moja ambalo hata Diamond mwenyewe hawezi kusahau katika
historia ya muziki wake, ni pale mama yake mzazi alipojitolea pete yake
ya dhahabu na kuiuza ili mwanaye ambaye ni Diamond apate hela ya kuingia
studio na kurekodi track yake ya kwanza.Naamini ni wazazi wachache sana wanaweza kufanya jambo kama hili, mbali na kupitia vizuizi vingi katika safari yake ya muziki, mama yake mzazi ndio aliyekuwa rafiki wake wa karibu aliyefanikiwa kumuongoza Diamond tena bila kukata tamaa, hadi hii leo kufikia mafanikio aliyonayo ambayo hata Raisi wa nchi yake(mH.Jakaya) hawezi kusahau jina la Diamond pale anapojarbu kuongelea sanaa ya muziki huu wa Tanzania. Ukaribu huo unaweza kuonekana ni umetoka mbali, ni zaidi ya mama, ni mtu ambaye amechangia mafanikio makubwa katika muziki wake.