Jafo aonya viongozi wa dini wanaofanya ubadhirifu

humph the GREAT
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo amewataka viongozi wa dini nchini kuwa waaaminifu kwenye matumizi ya fedha wanazopatiwa na wahisani kwa lengo la kusaidia jamii ya watanzania ambao ndiyo walengwa wa misaada hiyo.

Mhe Jaffo ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam kwenye mahojiano maalum kuhusu matumizi mabaya ya fedha ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na baadhi ya waumini, vitendo ambavyo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa dini ambao siyo waaminifu na kutumia fedha za misaada kutoka kwa wahisani kinyume na makubaliano.

Amesema kila kiongozi katika nafasi yake ahakikishe anasimamia haki na usawa ili kuhakikisha nchi inabadilika kuanzia ngazi za chini hadi ngazi ya serikali kuu, hivyo pia jamii ya watanzania inapaswa kushiriki katika kusimamia haki za watanzania wote zinafuatwa na kulindwa bila ubaguzi.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post