Mbwamwitu 22 wauawa Ngorongoro

humph the GREAT
Ngorongoro.Watu wanaodhaniwa ni wafugaji wamewauwa mbwamwitu 22 kwa sumu ndani ya eneo la Mamlaka a Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA), mkoani Arusha.

Wakizungumza na waandishi wa habari, mtafiti mwandamizi mradi wa  mbwamwitu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI), Dk Ernest Mjingo na kaimu mhifadhi Wa NCAA, Julius Kibebe walisema mbwamwitu hao, wameuawa katika kipindi cha miezi tisa.

Dk Mjingo  alisema Septemba 15 mwaka huu wamebaini kuuawa kwa mbwamwitu 11, katika eneo la bonde la Ngutotu katika kijiji cha Kakesyo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post