Samsung Galaxy Note7 Zapigwa Marufuku Kwenye Ndege

humph the GREAT

epa_samsung_note_7_ml_160902_12x5_1600

epa_samsung_note_7_ml_160902_12x5_1600Maafisa wa uchukuzi wa ndege nchini Marekani wamewatahadharisha abiria wanaosafiri kwa ndege kutofungulia au kuchaji simu za Samsung Galaxy Note 7 smartphones wakiwa ndani ya ndege.
Onyo hilo limetolewa ikiwa ni siku chache bada ya kuipotiwa kwa simu hizo kuwa zimekuwa zikiripuka aidha zikiwa zinachajiwa au mtumiaji akiwa anaongea au hata kama ikigusa sehemu yenye joto kidogo tu. Hii ni kutokana na aina za betri za simu hizoambazo zimetengenezwa kwa chaji (ions) zitokanazo na madini ya lithium (lithium-ion).
_91003684_gettyimages-588328896Taasisi ya Uchukuzi wa Ndege Marekani (FAA) pia imewashauri watu kutoweka simu hizo kwenye mizigo ambayo wanaingia nayo eneo wanamoketi abiria kwenye ndege. Taasisi hiyo imekuwa ikiendesha ukaguzi maalumkwenye mabegi ya abiria wake ili kugundua kama abiria amebeba Samsung Galaxy Note 7 au la!
_91003684_gettyimages-588328896
Kampuni ya Samsung ilisitisha uuzaji wa simu hizo na kukubali kwamba kulikuwa na hitilafu wakati wa uundaji wa betri za simu hizo. Kampuni hiyo hata hivyo ilisema ni vigumu kutambua ni simu gani zilizo na kasoro.
_90995808_burntnotearielgonzalezMashirika ya Australia ya Qantas na Virgin Australia pia yamewashauri wateja kutoweka chaji simu zao au hata kuzitumia wanaposafiri kwa ndege.
Mbali na kasoro hizo, simu hiyo ambayo ilizinduliwa mwezi uliopita imefurahiwa na wateja ambapo simu takriban 2.5 milioni za Note 7 zilikuwa zimesafirishwa maeneo mbalimbali duniani.
_90995808_burntnotearielgonzalez
Samsung wamesema wateja ambao tayari walikuwa wamenunua simu hizo, na zimepata hitilafu, watapewa fursa ya kuzibadilisha. Shughuli ya kupata simu mpya itachukua takriban wiki mbili.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post