humph the GREAT
"Mchana na usiku huzunguka kutani mwake; Uovu na taabu zimo ndani yake;
Tamaa mbaya zimo ndani yake; Dhuluma na hila haziondoki mitaani mwake.
Kwa maana aliyetukana si adui; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza
juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo, ningejificha asinione. Bali ni
wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana. Tulipeana
shauri tamu; na kutembea Nyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano."