humph the GREAT
Dotnata Awafuturisha Wasanii
Wasanii wa kike wakichukua futari.
Wasanii wa kiume wakipata futari.
Wasanii wakimfanyia Dotnata dua maalum.
Dotnata (katikati), mama Kanumba (kulia), Stara Thomas (kushoto) wakiwa katika pozi.
WASANII mbalimbali wa filamu Bongo, jana walipata fursa ya kushiriki futari na msanii mwenzao, Illuminata Poshi ‘Dotnata’ ambapo walikunywa na kunywa mfano wa sherehe ya harusi.
Wasanii hao walikula na kunywa nyumbani kwa mkongwe huyo wa filamu nchini, maeneo ya Ubungo, jijini Dar ambapo kila mualikwa alisikika akisifia jinsi walivyofurahia ‘mapochopocho’ hayo ya nguvu.
“Dah! Kweli huyu dada Mungu ambariki maana ametuandalia futari nzuri na ya nguvu na ukizingatia ni hivi karibuni tu alipata matatizo ya ajali lakini akaona ni vyema akae na kula pamoja nasi, huu ni upendo wa ajabu,” walisikika baadhi ya wasanii wakijadiliana.
Naye Dotnata aliwashukuru wasanii hao kuitikia wito wake na kushiriki naye futari na kusema kwamba kufuturisha siyo utajiri ni moyo wa mtu tu hivyo kuwataka wawe na umoja ili waweze kuwa na maendeleo katika tasnia ya filamu.

Tags
Burudani