humph the GREAT
Msimamo wa baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi juu ya kuizuia
Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifungo na Uvuvi ya mwaka
2017-2018 hadi pale watakapopata majibu yenye kueleweka juu ya hatua ya
rasilimali ya mchanga kuhodhiwa na Serikali badala ya wananchi wenyewe
kama ilivyokuwa awali utapata majibu leo wakati waziri wake, Hamad
Rashid atakapojibu hoja zao.
Hatua ya wajumbe hao imetokana na malalamiko ya wananchi waliokuwa
wakimiliki mashamba ambayo sasa yanachimbwa mchanga chini ya uangalizi
wa Serikali huku wao wakiambulia patupu.
Awali, mashamba hayo yalikuwa yapo chini ya wananachi ambao walikuwa
wakiyatumia kuvuna na kuuza mchanga huo kwa wamiliki wa magari na
kampuni mbalimbali za ujenzi.
Mwakilishi wa Mfenesini, Machano Othman Said alisema pamoja na
rasilimali hiyo kuonekana kupungua kwa kiwango kikubwa, haikusatahili
wananchi kupokonywa mashamba yao bila makubaliano maalumu.
Mwakilishi wa Kijitoupele, Ali Suleima Ali ‘Shihata’ alisema utaratibu
uliowekwa na Serikali juu ya mchanga ni hatari na unahitaji kufanyiwa
marejeo ili kuepusha athari zinazoweza kuepukika.
Tags
HABARI