humph the GREAT
Msanii
wa filamu nchini Yusuph Mlela aamemshutumu rapa Nay Wa Mitego kwa kile
anachodai kuwa msanii huyo anapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya
baadhi ya wasanii wa filamu nchini.
Baada
ya wasanii hao kuandamana wakipinga uingizwaji wa filamu za nje ambazo
hazilipi kodi, kwa madai ziwaaribia soko lao la filamu za ndani, rapa
Nay wa Mitego alisikika akisema kuwa baadhi ya wasanii wa filamu ambao
waliandamana ni mataahira kwani kitendo cha wao kutaka filamu za nje
zizuiliwe, hakina tija na mantiki yoyote.
“Walichokifanya
baadhi ya Bongo Movie mataahira ni sawa na sisi wasanii tugome kuimba
kisa nyimbo za wasanii wa nje zinapigwa sana Tanzania huyo ni utaahira,”
alisema Nay wa Mitego kupitia video ambayo ameisambaza mtandaoni.
Kutokana
na maneno ya kejeli ya Nay wa Mitego, muigizaji wa filamu Yusuph Mlela
alishindwa kuvumilia na kuamua kumtolea povu rapa huyo.
“Nay
True Boy wewe jamaa si ulikuwa chokoraa wewe, leo umeyapatia kidogo
unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa
waigizaji\wanamuziki wakubwa….Acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako
binafsi… sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka wanaozisambaza
wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo
la maandamano” aliandika Mlela Instagram.
Aliongeza,
“Nay wa Mitego acha kutafuta sifa… nakushangaa kuwa na ufikirivu mdogo
kama wewe siyo msanii…halafu huwezi kufananisha filamu na muziki….. Wewe
si mtoto wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za
boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie adabu…..
This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu ********** kuongea sana
tabia za kike, wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote
pale” Yusuph Mlela
Tags
Michezo na burudani