humph the GREAT
Msanii
wa filamu nchini, Jacob Steven maarufu kama JB amefunguka ya moyoni na
kusema kwamba ni kweli sinema zao zina mapungufu mengi lakini isiwe
sababu ya wao kuacha kudai haki zao wanazoamini kuwa wananyonywa katika
pato la mauzo.
Hayo
yameibuka baada ya kelele nyingi katika mitandao ya kijamii ikiwasema
waigizaji pamoja na watayarishaji wa filamu nchini kukosa ubunifu wa
kutosha na sasa kushinikiza serikali izuie kuingiza filamu zinazotoka
nje ya nchi.
“Kwenye
shida mimi sitajali nani ananisaidia ili mradi anagusa maslahi yangu,
ugali wangu. Nakiri sinema zetu zina mapungufu mengi lakini hilo siyo
sababu za kuacha kudai haki zetu, ni kama mgonjwa akiumwa leo anapelekwa
kwa mganga kesho anapelekwa kuombewa, anatetea roho yake”. Ameandika Jb
kupitia mtandao wake wa kijamii instagram
Vilevile
JB, amesema hakuna aliyesema filamu za nje zifungiwe ila wanachotaka ni
zifuate utaratibu kama wanavyofuata wao wenyewe.
“Ngoja
tumalize hili tusichanganye na pia hakuna aliyesema zifungiwe hapana
zifuate utaratibu kama sisi tunavyofuata hizo hizo ‘movie’ zetu mbovu
ndiyo zinatuwezesha kuishi lakini pia lazima mfahamu biashara hii ni
kubwa kuliko mnavyodhania, muvi mbili zinanitosha kuishi kwa mwaka
mzima, ushawaza ni kiasi gani ?”. Alisisitizia JB
Tags
Michezo na burudani
