Kampeni ya ‘Magufuli Baki’, Kutikisa Nchi Nzima

humph the GREAT
 Image result for magufuli 
Watanzania wote bila kujali jinsia, dini wala kabila wameshauriwa kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupigania rasilimali za wananchi wanyonge na masikini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Sengerema kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, Mabawa Laurence amesema :
“Nitazunguka nchi nzima kwa gharama zangu kupata fursa ya kuwasikiliza wananchi kupitia kampeni yangu ya ambayo inajulikana kwa ‘Magufuli Baki’ kuhakikisha wananchi wanatoa maoni yao juu ya Rais akimaliza kipindi chake ili aendelee ama la!”.


Mabawa Laurence akifafanua jambo.

Aidha alieleza kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wanasiasa na wananchi ambao hutoa lugha za maudhi na kejeli kwa baadhi ya Watanzania wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.

Amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 inatoa haki kwa kila Mtanzania kutoa maoni yake bila kuvunja katiba, kwa hiyo kitendo cha kushambuliwa kwa maneno makali ni kosa kisheria.
Hivyo kupitia kampeni aliyoianzisha itaweza kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao ambayo yatasambazwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post