Shabiki Hassan Omary, akiingia katika Uwanja wa Taifa.
Shabiki huyo anayefahamika kwa jina la Hassan Omary, aliingia katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Everton ilipokuwa ikipambana na Gor Mahia ya Kenya ukiwa ni mchezo maalum wa kirafiki ulioandaliwa na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa ambapo Everton iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Akiwa kamkumbatia Rooney.
“Kwa kweli nilipanga kufanya tukio lile, ila kwa sasa siwezi kuzungumza zaidi, kesho (leo Jumatatu) nitakuja ofisini kwenu na nitazungumza yote kupitia runinga yenu ya Global TV Online ili watu wengi waweze kuniona na kunisikia,” alisema shabiki huyo. Subscribe Hapa www.youtube.com/user/uwazi1
Stori: Ibrahim Mussa na Abdallah Zalala | Championi
0 Comments