humph the GREAT
Mbunge wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF) amezua vicheko bungeni baada
ya kuuliza swali ambalo linalohoji tafiti zinaonyesha kwamba wanaume
waliotahiriwa wanakuwa active zaidi na wananogesha zaidi yale mambo
(mapenzi).
Mbunge Khatibu ameuliza swali hilo leo bungeni mjini Dodoma, ambapo
spika Ndugai alipinga kuwa hilo sio swali “hilo nalifuta sio swali sio
swali” amesema Spika Ndugai.
“Tafiti zinaonyesha kwamba wanaume waliotahiriwa wanakuwa active zaidi
na wananogesha zaidi yale mambo, Je Mhe. Spika katika hali hiyo wabunge
wanawake kupitia bunge hili mtoe kidogo ushahidi wa haya wanaume
waliokuwa hawajatahiriwa waige mfano huo?
alihoji Mbunge Khatibu.
0 Comments