Jaji katika jimbo la Michigan anasema idadi ya waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya daktari wa zamani wa timu ya mazoezi ya viungo ya Marekani, Larry Nassar, imeongezeka mpaka kufikia 265.
Mpaka sasa Dkt Larry amekwisha hukumiwa kwa makosa zaidi mia moja na sabini na tano baada ya baada ya kuhukumiwa kwa makosa kumi ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wasichana na wanawake wadogo, wakiwemo wale wanaoshiriki michuano ya Olimpiki.
Nassar anafikishwa mahakamani kwa mara nyingine tena kwa makosa ya kudhalilisha wagonjwa katika chumba cha nyuma cha klabu ya mazoezi ya viungo huko Michigan.
Bodi nzima ya wana mazoezi ya viungo ya Marekani sasa imejiuzulu juu ya kushindwa kwake kulinda wanasarakasi vijana dhidi ya daktari huyo, ambaye ameelezewa kuwa labda mnyanyasaji mkubwa wa kijinsia dhidi ya watoto katika historia.
Wiki iliyopita, Lasser alihukumiwa kwenda jela miaka 175 baada ya kukutwa na makosa ya ukatili wa kingono dhidi wananawake na wana michezo.
Katika kesi hiyo mashahidi 160 waliwasilisha ushahidi wao huku Nasser mwenyewe alikiri makosa kumi.
Alikuwa tayari akitumikia kifungo cha miaka 60 kutokana na kukutwa na hatia ya kumiliki picha ngono za watoto kinyume cha sheria.
Jaji Rosemary Aquilina aliiambia mahakama kuwa alijisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na kwamba anataka iwe fundisho kwa wengine.
Takriban wasichana 140 waliwasilisha kesi dhidi ya Nassar, taasisi ya USA Gymnastics na chuo kikuu cha MSU, wakidai kuwa taasisi hizo mbili zilipokea taarifa tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya daktari huyo miaka kadhaa ya nyuma lakini hazikuchukua hatua zozote.
Taasisi hiyo ya michezo na chuo hicho zimekana kuwa kulikuwa na chochote cha kufichwa.
Hukumu ya Larry Naser ilifuatia wiki ya ushuhuda kutoka kwa wanawake takribani mia moja na sitini, wakiwemo washindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki Biles, Aly Raisman, Gabby Douglas na McKayla Maroney
0 Comments