Manchester united na Chelsea wapigwa ligi kuu england

humph the GREAT
Alli appeared to be fouled by Antonio Valencia with the score at 2-0 in the first halfHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlli alionekana kuchezewa vibaya na Antonio Valencia mabao yakiwa 2-0 kipindi cha kwanza
Meneja Mauricio Pochettino aliwasifu sana vijana wake wa Tottenham kwa kuanza mechi kwa ukali baada ya Christian Eriksen kufunga bao sekunde 11 pekee baada ya mechi kuanza, na kufanikiwa kulaza Manchester United 2-0 uwanjani Wembley.
Ilikuwa siku ya miamba kulala kwani mabingwa watetezi Chelsea pia walilazwa 3-0 na Bournemouth, ushindi ambao meneja wao Eddie Howe ameueleza kuwa matokeo bora zaidi kwao Ligi ya Premia.
Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Callum Wilson, Junior Stanislas na Nathan Ake yaliwahakikishia Bournemouth ushindi wao wa kwanza ugenini katika mechi saba za ligi, Chelsea nao wakaondoka uwanjani na kichapo kilichofikia kipigo kikubwa zaidi walichopokezwa msimu huu.
Bournemouth, ambao wanacheza ligi kuu msimu wa tatu pia walilaza Chelsea na Manchester United msimu wa 2015-16, Liverpool na Leicester msimu wa 2016-17 na Arsenal mapema mwezi huu.
Uwanjani Wembley, raia wa Denmark Ericksen alifikia mpira kutoka kwa Harry Kane na Dele Alli na kufunga bao ambalo kwa sasa ni miongoni mwa mabao ya tatu katika kufungwa kwa kasi zaidi Ligi ya Premia.
United walijibu vyema kujipata nyuma na karibu Jesse Lingard asawazishe lakini Phil Jones akaelekeza krosi ya Kieran Trippier na kujifunga dakika ya 28 na kuwaweka Spurs mabao mawili mbele.
"Unaweza kushinda mechi iwapo uko tayari kupambana. Ilitufaa sana kuanza vyema mechi," alisema Pochettino.
Meneja wa United Jose Mourinho alieleza bao hilo la kwanza kuwa "la kushangaza", na akaongeza kwamba: "Bao la pili kiakili huiua timu.
"Ili kushinda mechi timu inahitaji kufunga mabao na kujilinda vyema - wakati tulikuwa hafifu sana."
Kushindwa huko kulifikisha kikomo mkimbio wa United wa kutoshindwa mechi nane ligini na pia kupanua mwanya kati yao na viongozi Manchester United hadi alama 15.
Eriksen returned to the side after injury and needed just 11 seconds to find the netHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionChristian Eriksen alifunga bao la kwanza sekunde 11 baada ya mechi kuanza
Alexis Sanchez hakuonekana kuwafaa sana mashetani hao wekundi.
Hakushambulia goli la wapinzani na aliugusa mpira mara mbili pekee eneo la hatari la Tottenham.
Mourinho lost Marouane Fellaini to injury seven minutes after sending him onHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMarouane Fellaini alilazimika kuondoka uwanjani dakika saba baada ya kuingia uwanjani
Eriksen dictated and offered Tottenham moments of calm in an otherwise frenzied encounter. His accuracy in possession, his weight of pass and desire to constantly make things happen proved telling throughout. Only Kieran Tripper touched the ball more of all the players on the pitch and Eriksen mixed passes with crossing as his eight crosses was a game high.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEriksen aliwafaa sana Tottenham
Manchester United watakuwa wenyeji wa Huddersfield Jumamosi 15:00 GMT nao Tottenham wasafiri Anfield kukutana na Liverpool siku moja baadaye (16:30).
Callum WilsonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionCallum Wilson alifunga bao la nne katika mechi saba Bournemouth
ChelseaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMchezaji wa zamani wa Arsenal Olivier Giroud na beki Emerson Palmieri kutoka Roma aliyenunuliwa £17.6m walitambulishwa uwanjani wakati wa mapumziko
Bournemouth watarejea kucheza EPL Jumamosi 3 Februari kwa mechi ya nyumbani dhidi ya Stoke (15:00 GMT).
Olivier Giroud na Emerson Palmieri nao huenda wakachezea Chelsea mara ya kwanza Jumatatu 5 Februari (20:00 GMT) vijana hao wa Conte watakapokutana Watford uwanjani Vicarage Road.

Matokeo kamili ya mechi za Jumatano

  • Chelsea0 -3 Bournemouth
  • Everton2 -1 Leicester
  • Newcastle 1 - 1 Burnley
  • Southampton 1 -1 Brighton
  • Man City 3 -0 West Brom
  • Stoke 0-0 Watford
  • Tottenham 2-0 Man Utd

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post