Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Jua historia ya mlima Kilimanjaro na maajabu yake part 01

humph the GREAT

Kilimanjaro (Volkeno)

Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi
Kilele cha Kibo kwenye mlima Kilimanjaro
Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote baraniAfrika. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa mita5,895 (futi 19,340).
Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hii mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima.
Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko mnamo mwaka 1730.
Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru. Mtu wa kwanza wa kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangualiyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kwa Kijerumani:Kilele cha Kaisari Wilhelm)kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.
Kibo ina theluji na barafuto ndogo kadhaa.

Jina

Ramani ya 1888 inayoonyesha jina "Kilima-Ndscharo" katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Asili ya jina "Kilimanjaro" haijulikani kikamilifu. Vyanzo vya kimaandishi vinajulikana tangu takriban mwaka 1860 ambako wapelelezi wazungu walitumia jina hili katika taarifa zao wakidai "Kilimanjaro" ilikuwa jina la Kiswahili.[1] Pamoja na umbo hili kulikuwa pia na tahajia ya sehemu mbili ama "Kilima-Njaro"[2] au kwa namna ya Kijerumani “Kilima-Ndscharo”.
Johann Ludwig Krapf aliandika mnamo 1860kuwa Waswahili kwenye pwani waliita mlima huu "Kilimanjaro". Alisema pia ya kwamba hao Waswahili walieleza maana yake kuwa ama “mlima mkubwa” au “mlima wa misafara” ingawa mwenyewe hakukubali maelezo haya. Kwa elezo la mwisho "Kilima" kilimaanisha "mlima" na "Jaro" labda "misafara".[1]
Jim Thompson aliandika mnamo 1885 kuwa jina Kilima-Njaro lilichukuliwa mara nyingi kuwa na maana ya "mlima mkubwa" lakini mwenyewe alipendelea maeelzo tofaiti yalyosema "mlima mweupe". [3] "Njaro" ni Kiswahili cha Zamani kwa "ng’ara".[4] Vivzo hivzo Krapf aliandika za kwamba aliwahi kuwatembela Wakamba mnamo 1849 walioit mlima “Kima jaJeu” yaani mlima mweupe [5]Leo hii Wakamba wangesema “Kiima Kyeu” na elezo hili limekubaliwa na watafiti mbalimbali.
Wengine huona ya kwamba ni wazungu wasiojua Kiswahili vema waliochanganya “mlima” na “Kilima”.
Wengine wamejaribu kuona msingi wa jina katika lugha ya Kichagga. Hapa wanadai uwezekano kuwa "Kileman" imetokana na neon la Kichagaa "kileme" inayomaanisha “kinachoshinda” au neno "kilelema" inayomaanisha "kilichokuwa vigumu, kilichoshindikana". Katika hoja hili "Jaro" imetokana na Kichagga “njaare” (aina ya ndege, au kufuatana na wengine chui) au kutoka neno “jyaro” (msafara). Elezo nyingine ni ya kwamba Wachagga walisema mlima huu ni hauwezi kupandwa "kilemanjaare" au "kilemajyaro" na wapakazi au wafasiri kutoka pwani waliichukua kuwa jina la mlima na kutafsiri vile kwa wazungu.
Tangu miaka ya 1880 mlima umekuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumaniukaitwa "Kilima-Ndscharo" kwa Kijerumani.[6]
Tarehe 6 Oktoba 1889 Hans Meyer alikuwa mtu wa kwanza anayejulkikana kupanda mlima na kufika hadi kilele cha Kibo. Alichagua jina la "Kaiser-Wilhelm-Spitze" ("Ncha ya Kaisari Wilhelm"[7]).[8] That name apparently was used until Tanzania was formed in 1964,[9] when the summit was renamed "Uhuru", meaning "Freedom Peak" in Kiswahili.[10]

Post a Comment

0 Comments