Maradona yamkuta makubwa kisa kumtusi trumph

humph the GREAT

NYOTA wa zamani wa soka nchini Argentina, Digo Maradona amenyimwa kibali cha kuingia nchini Marekani baada ya kudaiwa ‘kumtusi’ rais wa nchi hiyo, Donald Trump kupitia runinga.

Maradona alitarajiwa kusafiri kuelekea Miami kushiriki katika kusikilizwa kwa kesi ya mkewe wa zamani, lakini Maradona ambaye anasimamia Klabu ya UAE ya Al Fujairah amekatazwa visa kwa mara nyengine kuingia Marekani.

Katika mahojiano Maradona anadaiwa kumuita Trump ‘Chirolita’. Neno hilo ni tusi linalojulikana sana nchini Argentina likimaanisha watu ambao ni vikaragosi.Wakili wa Mardona Matias Morla sasa atamwakilisha mteja wake katika kesi hiyo mjini Miami.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post