humph the GREAT
Jumanne ya March 6 2018 club ya Yangailicheza mchezo wake wa kwanza wa round ya kwanza wa michuano ya Club Bingwa Afrika dhidi ya wageni wao Township Rollers, mchezo uliyochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku mchezo wa marudiano ukiropotiwa kuwa utachezwa siku 10 zijazo.
Yanga wakiwa nyumbani wamepata bahati mbaya na kujikuta wakiweka rehani tiketi yao ya kushiriki michuano ya club Bingwa Afrika hatua ya makundi, baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa wageni wao Township Rollers, baada ya game kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa aliridhia kuongea na waandishi wa habari.
“Tumepoteza lakini hiki ni kipindi kimoja na naimani mechi ya ugenini tunaweza tukapata matokeo vile vile, kwa sababu wenyewe wamecheza hapa wamepata matokeo kwa hiyo hata sisi tutarudi tutajiandaa, tutajaribu kurekebisha makosa yetu sababu tumeona kuwa na wao wanafungika pia”>>> Shadrack Nsajigwa
Tags
Michezo na burudani