Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

dogo janja awachana wanaume

humph the GREAT

Mwanamke Hata Awe na Pesa Kiasi Gani Hawezi Kumpenda Mwanaume Asiye na Muelekeo- Dogo Janja
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abubakar Chande maarufu kama 'Dogo Janja' ambaye pia ni mume wa msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kudai mwanamke hata awe na pesa kiasi gani hawezi kupenda mwanaume asiyekuwa na muelekeo wa maisha.


Dogo Janja ametoa kauli hiyo siku za hivi karibuni wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha DADAZ kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi 6:00 mchana baada ya kuulizwa kuwa ni kweli wanaume wengi wanaogopa kuwa na wanawake waliowazi kipato.

"Mwanamke hata awe na hela vipi hawezi kuwa na mwanaume asiye na muelekeo kwani mara nyingi huwa wanapenda akiwa na rafiki zao basi awe 'proud' na mtu aliyenae", amesema Dogo Janja.

Pamoja na hayo, Dogo Janja ameendelea kwa kusisitizia baadhi ya mambo kuwa "wanaume wanapaswa wawe 'real' yani wawazi katika mahusiano yao na sio kuishi katika maisha ya kujidanganya, kwani inaweza kuwapelekea kupata hasara na kuumbuka".

Post a Comment

0 Comments