humph the GREAT
STAA wa filamu Bongo, Jennifer
Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa ‘ukauzu’ wa kufanya jambo bila kumhofia
mtu ndio umemfanya afike mbali kimaisha.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Odama alisema kuwa kuna watu
wengi hasa mastaa wanaogopa macho ya watu hivyo hata kama wapo kwenye
shida fulani wanajivunga tu na kujisababishia matatizo mengine kwa
kushindwa kuikubali au kuipokea hali ambayo wanakutana nayo kwa kipindi
hicho.
“Mimi jamani ningekuwa naogopa macho ya watu basi nisingesonga mbele
kabisa lakini sikujali na hata nikianguka siangalii mtu ameniangaliaje,
napambana kuinuka upya,” alisema Odama.
Mrembo huyo ni miongoni mwa warembo wachache Bongo ambao wanamiliki
kampuni binafsi ya kuzalisha filamu, kampuni yake inaitwa J-Film 4 Life.
0 Comments