Haki miliki ya pichaISTOCKImage captionPamoja na kuwepo kwa mazingira magumu, historia inaonyesha wanawake waliishi muda mrefu zaidi
Wanawake nndio jinsia yenye nguvu kuliko wanaume.
Bila shaka wengi wenu mtakuwa mlishalifikiria hili ingawa bila kuamini kabisa, lakini sasa hapa kuna utafiti wa kisayansi wa kuthibitisha hilo.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa katika mazingira magumu kama vile ya njaa, milipuko ya magonjwa na utumwa, wanawake wanaweza kuishi muda mrefu zaidi kuliko wanaume.
Wanawake huishi kwa muda mrefu katika mazingira mengi, wanawake wa Kiingereza huishi mpaka miaka 83.1 ukilinganisha na wanaume miaka 79.5, Scotland miaka 82.1 kwa wanawake na wanaume miaka 77.1.
Wasomi kutoka chuo cha Southern cha Denmark wamezitazama data kutoka katika matukio saba ya kihistoria ambapo watu walipitia mazingira magumu , ili kupata utofauti.
Maswala yaliyoangaliwa ni pamoja na njaa iliyoikumba jamii ya Ireland mwaka 1845-1849, maradhi ya surua na maisha waliyoyapitia watumwa wa Liberia waliokuwa wakirejea Afrika kutoka Marekani mwanzoni mwa karne ya 19.
Changamoto hizi zilisababisha kupungua kwa umri wa kuishi.
Wakati yalipotokea maradhi ya surua mwaka 1882 Iceland, kwa mfano umri wa kuishi ulipungua kutoka miaka 43.99 mpaka18.83 kwa wanawake na kutoka miaka 37.62 mpaka miaka 16.76 kwa wanaume.
Watafiti walibaini kuwa tofauti ya jinsia kwenye vifo vya watoto wachanga ''kulichangia sana'' tofauti kati ya umri wa kuishi kwa wanawake na wanaume, ikionyesha kuwa ''watoto wachanga wa kike waliweza kuishi kwenye mazingira hatari kuliko watoto wachanga wa kiume''.
Kutegemea majibu ya utafiti huu, wasomi walihitimisha, ''kwa nadharia kuwa kuishi muda mrefu kwenye mazingira magumu kwa wanawake kunatokana na sababu za msingi za kibaiolojia, jinsia ya kike inaishi muda mrefu kuliko ya kiume hata katika hali ya umri mchanga.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wataalam hao wamesema tofauti ya homoni pia ni sababu ya kuwepo tofauti hiyo, mfano wanawake kuwa na homoni nyingi za kiume, kuna athari ya vichochezi wakati homoni za kiume , zikikutwa kwa wingi kwa mwanaume, kunaweza kuathiri mfumo wa kinga mwilini.
Mwandishi wa jarida la PNAS, Profesa Virginia Zarulli aliandika '' Mazingira waliyoyapitia watu yalikuwa ya kutisha.Ingawa mabalaa hayo yalipunguza uwezo wa kuishi kwa wanawake, wanawake waliishi muda mrefu zaidi kuliko wanaume.''