humph the GREAT
ARSENAL ipo katika hatari ya kupoteza mastaa wake sita kutokana na kukwama kuwaongeza mikataba yao.
Kufuatia hali hiyo huenda Arsenal it-alazimika kuwauza mastaa hao ambao miongoni mwao ni Pierre-Emerick Aubameyang, Mezut Ozil na Laurent Koscielny ili kuwawahi kabla ya mikataba yao kumalizika, Arsenal inakabiliwa na tishio la kupoteza mastaa sita bila ya kupata chochote ikiwa hawataharakisha kumaliziana nao juu ya suala la mikataba.
Mkurugenzi Mkuu wa Arsenal, Vinai Venkatesham alijiapiza juzi kuwa klabu hiyo itahakikisha inaepuka ishu ya Aaron Ramsey haitokei tena,
Arsenal ilishindwa kufikia muafaka na Ramsey juu ya kuongeza mkataba mpya na matokeo yake anajiunga na Juventus bila ya klabu hiyo kuambulia chochote.
Venkatesham amedai kuwa klabu hiyo itahakikisha inaweka sawa masuala yote ya mikataba ya mastaa wake sita ambao mikataba yao inakaribia kumalizika.
Alionya kuwa mastaa wanaomaliza mikataba yao hadi mwaka 2021 basi watauzwa ikiwa watashindwa kufikia muafaka na klabu.
“Ikitokea tumeshindwa kufikia muafaka na wachezaji wetu hawa basi watauzwa fasta ili fedha itakayopatikana inunue wachezaji wengine.
Klabu inatakiwa kuwa makini katika suala la kushughulika na wachezaji wanaokaribia kumaliza mikataba nasi,” alisema Venkatesham.
Miongoni mwa mastaa walio hatarini kuuzwa ni pamoja na nahodha Koscielny, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2020.
Ikiwa klabu hiyo itashindwa kuelewana naye kabla ya Januari, mwakani ina maana klabu nyingine zinaweza kuzungumza naye.
Naye mfungaji tegemeo wa Arsenal, Aubameyang, ambaye mkataba wake unaisha mwaka 2021, naye zinahitajika jitihada za kuhakikisha anabakia katika timu hiyo.
Mesut Ozil, ambaye ni mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Arsenal akipata pauni 350,000 kwa wiki naye anamaliza mkataba wake mwaka 2021 pamoja na Sokratis Papastathopoulos, Shkodran Mustafi na Henrikh Mkhitaryan
Mezut Ozil.

Tags
Michezo na burudani