humph the GREAT

Baada ya maelezo ya Stephen Masele, Spika Ndugai alisema kuwa Masele haelewi kinachoendelea kwani Masele hakuitwa kwa sababu ya jambo lolote kule PAP
Amesema Masele aliitwa nyumbani( Tanzania) kwa kuwa aliwaandikia viongozi wa juu kabisa “ujumbe wa ajabu” na aligonganisha mihimili. Spika Ndugai alisisitiza kuwa ingawa Masele alitumiwa ujumbe siku tatu tofauti kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, pamoja na njia ya WhatsApp lakini alikaidi.
“Tumekuita kwa sababu ya tabia mbaya, tatizo lako ni uongo, kugonganisha viongozi, fitina na uchonganishi. Binafsi nimesononeka sana na naendelea kusononeka” ameeleza Spika Ndugai.
Baada ya Maelezo Spika Ndugai aliwaomba wabunge kumpuuza na Kumsamehe Stephen Masele
“Bunge katika kuendeshwa kwake unaangalia mabunge mengine na mambo yaliyotokea huko nyuma. Yaliwahi kutokea mambo kama haya alipokuwepo Mzee Sitta, katika mazingira kama haya aliwahi kuliomba bunge limpuuze mbunge fulani. Kwa maana hiyo mimi nawaombeni sana tumpuuze Masele na tumsamehe.
Baada ya kukamilika kwa suala hili Spika Ndugai alimpisha Mwenyekiti wa Bunge, Azan Zunge aendelee kuongoza Bunge ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii amewasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo”

Tags
HABARI