humph the GREAT
Wanawake ambao wamewahi kupotea uja
uzito au waliovuja damu katika miezi ya awali ya uja uzito wanaweza
kuimarisha nafasi yao kujifungua salama iwapo watapewa homoni ya
progesterone, utafiti unaonyesha.
Watafiti nchini Uingereza wamefanya majaribio kwa wanawake 4000 wenye mimba.
Samantha
Allen, mwenye umri wa miaka 31, alianza kuvuja damu alipompoteza
mwanawe wa kwanza na alifanya hivyo tena alipokuwa mja mzito kwa mara ya
pili.
Badaa ya kupewa homoni hiyo kwa wiki naneo, almzaa mwanawe wa kiume Noah.
Progesterone ni homoni muhimu wakati wa uja uzito - inayotumika kuimarisha uzio wa kizazi ambako sehemu ambako kijusi kinajiambatanisha na kusaidia mfumo wa kinga mwilini.
Samantha alipewa tembe za homoni ya progesterone
kwa majaribio , ambazo alizitumia mara mbili kwa siku mapaka
alipotimiza wiki 16 za uja uzito.
Alisema aliacha kuvuja damu wiki moja tangu aaanze kutumia tembe hizo na aliendelea vizuri na uja uzito wake.
"Natumai hawatoteseka tena, inakuathiri sana," amesema.
Mwanamke
mmoja kati ya watano hupoteza mimba, na mara nyingi uvujaji damu
unahusishwa na kuongezeka hatari ya mwanamke kupoteza uja uzito.
wakati
homni hiyotayari imetumika katika mfumo wa kupachika mimba, IVF,
Samantha anasema hakuwa na shida yoyote kushiriki katika utafiti huo.
"Ninafurahi, sikuhisi hatari yoyote kwasbabu yalikuwa hayakuwa majaribio ya kiwango cha awali."
Utafiti huo wa chuo kikuu cha Birmingham
uliochapishwa katika jarida la afya la New England, umewahusisha kundi
la wanawake 200 waja wazito waliopewa homoni ya progesterone, huku kundi
jingine la wanaawake kama hao wakipewa tembe bandia.
Wote walikuwa wanavuja damu katika miezi ya kwanza ya uja uzito.
Licha ya kamba utafiti huo umeonyesha sio wanawake wote wanaovuja
damu katika siku za kwanza wanaweza kusaidiwa kwa kutumia homoni hiyo,
manufaa hayoni makubwa miongoni mwa wanawake walio na historia ya
kupoteza uja uzito. (Watoto watatu au zaidi)
Miongoni mwa wanawake
hao, kulikuwa na ongezeko la 15% la wanawake waliojifungua - huku 98
kati ya 137 wakifanikiwa kujifungua ikilinganihswa na 85 kati ya 148
waliopewa tembe hizo bandia.
Arri Coomarasamy, daktari wa afya ya
uzazi katika hospitali ya akina mama na watoto Birmingham amesema
matibabu hayo huenda yakasaidia kuokoa maisha ya maelfu ya watoto.
Ameendelea
kueleza kwamba matibabu hayo hatahivyo hayatofanya kazi kwa wanawake
wanaopteza uja uzito, kwasababu kuna sababu nyingi na ngumu kuhusu
kwanini wanawake hupoteza uja uzito.
Ni wanawake walio na tatizo la upungufu wa homoni ndio wanaoweza kufaidika.
Serikali ya Tanzania haitaongeza muda wa likizo ya uzazi , limeripoti gazeti la binafsi la The Citizen nchini humo.
Naibu
waziri wa afya Faustin Ndugulile ameliambia bunge kuwa wanawake
wanaojifungua mtoto mmoja wataendela kupewa 84 za likizo ya uzazi huku
wanaojifungua watoto mapacha wakipata likizo ya siku 100, limeeleza
gazeti hilo.
Dr Ndugulile alikuwa akijibu swali kutoka kwa Mbunge
wa chama kikuu cha upinzani Chadema Grace Tendega Jumanne ambaye
aliiuliza serikali iwapo ina mipango ya kuongeza siku za likizo kwa
akinamamawanaojifungua watoto njiti, linasema gazeti hilo
linalochapishwa kiola siku.
Naibu waziri alisema kuwa wanawake
wanaonyonyesha watapewa saa mbili kwa siku na kwamba serikali
itaendelea kutekeleza sera yake ya afya ya mwaka 2007 juu ya vipengele
vya huduma bure za afya kwa makundi maalumu, wakiwemo wanawake
wajawazito , limesema The Citizens.
Je gharama ya uzazi katika baadhi ya mataifa Afrika mashariki ikoje?
Kwa
mujibu wa shirika la afya duniani WHO, takriban wanawake 830 hufariki
kutokana na sababu zinazoweza kuepukika zinazohusiana na uja uzito na
kujifungua ikiwemo gharama za kupokea hudumu za afya.
99% ya vifo hivyo vyote hutokea katika mataifa yanayoendelea. Je hali iko vipi kwa baadhi ya maatifa ya Afrika mashariki?
Kenya:
Kenya
imekuwa ikishuhudia kiwango kikubwa cha vifo vya akina mama waja
wazito. Kutokana na hilo serikali iliidhinisha sera ya utoaji huduma za
bure kwa kina mama wanaojifungua katika taasisi za umma tagu Juni 2013.
Sera hii imekuwa ikiwawezesha wanawake waja wazito kupata huduma za bure wakati wa kujifungua katika vituo vya afya vya umma.
Mpango
uliopo ni kwamba vituo hivyo vya afya hutoa huduma ya bure na baadaye
serikali inavilipa kupitia wizara ya afya kulingana na idadi ya akina
mama waliozalishwa.
Pia hakuna malipo yanayotolewa kwa huduma za kabla na baada ya kujifungua kwa akina mama na watoto kwa hadi wiki sita.
Licha
ya huduma hiyo ya bure,kiwango cha hudumu zinazotolewa bado kinazusha
maswali mengi huku baadhi ya wazazi katika hospitali hizo za umma
wakiishia kujifungua katika hali duni na wengine hata kuishia kulala
kitanda kimoja na wazazi wenzao.
Sio wengi wanaoweza kumudu gharama za hospitali za kibinafsi nchini.
Uganda:
Suala
moja kubwa linalohusiana na afya ya uzazi ni nafasi ya akina mama
kufikia huduma za dharura na za kiwango bora za uzazi na changamoto
nyinginezo kwa wanawake nchini Uganda kufikia huduma hizi, zikiwemo
gharama kubwa. Kama nchi nyingine nyingi zinazoendelea, Uganda
inashuhudia kiwango kikubwa cha akina mama wanaofariki wakati wa
kujifungua - jambo linalodhihirisha ufikiwaji wa huduma hizo za afya.
Hata
wakati huduma hizo zinapatikana, kwa kawaida idadi ya wahudumu, dawa na
vifaa hospitalini inakuwa ndogo ikilinganishwana idadi ya akina mama
wanaohitaji hudumu hiyo.
Muongozo uliotolewa na shirika la Afya
duniani ni kwamba mkunga mmoja anastahili kuwazalisha takriban wanawake
175 kwa mwaka, lakini wakunga nchini Uganda huwazalisha kati ya akina
mama 350 hadi 500 kwa mwaka.
Upungufu na usambazaji mbovu wa wahudumu wa afya unaathiri kwa jumla gharama ya huduma ya afya ya uzazi na watoto.
Tanzania:
Idadi
ya wanawake wanaofariki wakati wa uja uzito na kujifungua nchini
Tanzania, kati ya 454 kwa kila visa 100,000 vya kujifungua - ni miongoni
mwa zilizo kubwa duniani.
Licha ya kwamba serikali imeahidi kuisaidia hali, idadi hiyo ya vifo haijapungua
0 Comments