Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za soka ulaya

humph the GREAT
Tetesi za soka Ulaya 28.09.2019: Eriksen, Pogba, Neymar, Mourinho, Higuain, Sane

Paul POgba
Paul Pogba ameiomba Man United kumpatia kandarasi mpya yenye thamni ya £600,000 kwa wiki . Kiungo huyo wa kati wa Ufaransa ,26, anajua kwamba ananyatiwa na Juventus pamoja na Real Madrid. (Tuttosport - in Italian)
Wachezaji wa Spurs wamekasirishwa na mkufunzi Mauricio Pochettino baada ya kusema kwamba walikuwa na ajenda tofauti wakati waliposhindwa na Colchester katika kombe la Carabao siku ya Jumanne.. (sun)
Manchester United inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27, huku Spurs ikijiandaa kutokosa huduma za kiungo huyo wa Denmark katika uhamisho wa bure mwisho wa msimu huu. (Goal)
Manchester United inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27
Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar na klabu yake ya zamani Barcelona bado hawajatatua mzozo kuhusu malipo ya uaminifu baada ya makubaliano ya kuzuia kuipeleka kesi hiyo mbele ya jopo la mahakama kugonga mwamba.. (Sky Sports)
Mawakili wanaomwakilisha Neymar na Barcelona wameafikia siku nyengine ya pili mnamo tarehe 21 Oktoba.. (ESPN)
Mchezaji wa Brazil Neymar, 27, alikuwa tayari kufutilia mbali kesi hiyo iwapo Barcelona ingejitolea kwa maandishi kumsaini tena. (Cadena SER - in Spanish)
Neymar JR
Mkufunzi wa Jose Mourinho anataka kurudi Real Madrid, baada ya kukataa ofa kutoka Monaco, Lille, Wolfsburg, Schalke na AC Milantangu alipofutwa kazi na klabu ya Manchester United mwaka uliopita . (Goal)
Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer amemchagua skauti wake wa kibinafsi kutazama wachezaji anaowalenga katika dirisha la uhamisho. (Sun)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kwamba hana wasiwasi kuhusu hali ya kiungo wa kati wa timu hiyo James Milner, 33, kuwa katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake . (Guardian)
Mkataba wa sare mpya ya Liverpool inayodhaminiwa na kampuni ya sare za michezo una thamani wa £15m kwa mwaka chini ya mktaba wao sasa na kmapuni ya New Balance, ambayo inatoa £45m kwa mwaka. (Times)
Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Gonzalo Higuain, 31, ametoa ishara ya kutaka kurudi katika klabu yake ya zamani ya River Plate kandarasi yake itakapokamilika 2021. (Fox Sports Radio Argentina - in Spanish)
Rais wa Bayern Munich Uli Hoeness anasema kwamba huenda klabu yake ikaimarisha upya hamu yake ya kutaka kumsajili winga wa ujerumani na Manchester City Leroy Sane, 23, mwezi Januari. (Planet Futbol via Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21, anasema kwamba alivutiwa na hamu kutoka man United msimu huu lakini anasisitiza kuwa makubaliano yoyote yatategemea klabu zote mbili.. (Times - subscription required)
Southampton na Manchester City zinamnyatia beki wa klabu ya Hearts mwenye umri wa miaka 17Aaron Hickey. (Daily Record)

Post a Comment

0 Comments