humph the GREAT
Kuna mgogoro wa kisiasa nchini marekani unaomuhusu rais Donald Trump, raia wa kigeniu, maswala kuhusu maadili na madai kuhusu wapinzani wa kisiasa na yote haya yamesababisha kushtakiwa bungeni kwa rais Trump. Habari hii inaweza kuwa ngumu kuelewa hivuyobasi haya hapa majibu ya maswali magumu.
Kwa nini haya ni muhimu?
Wakosoaji wa rais Trump wanmtuhumu kwa kutumiauwezo wake wa urais kuilazimu Ukraini kuchunguza kuhusu habari mbaya za mpinzani wake wa kisiasa Mgombea wa chama cha Demovrat Joe Biden.

Bwana Biden yuko kifua mbele kama mgombea wa chama cha Democrat kukabiliana na bwana Trump mwaka ujao.
Kwa upande mwengine , rais Trump yuko 'motoni'
Je mgogoro huu ulianza vipi?
Rais Trump na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky walifanya mazungumzo ya simu tarehe 25 mwezi Julai mwaka huu.
Katika mazungumzo hayo rais Trump anaonekana alimshinikiza mwenzake wa Ukraine kuwachunguza makamu wa rais wa zamani wa Marekani Joe Biden na mwanawe ambaye alikuwa mwanachama wa bodi ya kampuni inayomilikiwa na mfanyabiashara mmoja tajiri mwenye ushawishi wa kisiasa.
Simu hiyo ilipigwa baada ya utawala wa rais Trump kuchelewesha ufadhili wa kijeshi wa Ukraine katikati ya mwezi Septemba.
Bwana Trump pia alizungumzia kuhusu udukuzi uliofanyiwa barua pepe za chama cha Democrat katika simu hiyo ya Zelensky na kudai kwamba sava yake bado ipo mahala fulani nchini Ukraine.
Rais Trump anasema kwamba hajafanya makosa yoyote akitaja ukosoaji wake bungeni kama mzaha mkubwa.
Alikishutumu chama cha Democrat kwa kumtishia rais Zelensky kuzuia kura yao kuhusu sheria za Marekani zinazoathiria Ukraine na kusema kwamba mgogoro huo ulifanyika ili kutopatia kipau mbele mkutano wa bwana Trump katika Umoja wa matifa.
Je wanasiasa wengine wanasemaje?
Wabunge wa chama cha Democrats katika bunge la Congress wanasema kwamba simu hiyo iliofichuliwa ni thibitisho kwamba bwana Trump alitoa shinikizo kwa taifa jingine kwa manufaa yake ya kibinafsi.
Democrats wanasema rais alitaka Ukraine kuanzisha uchunguzi kuhusu ufisadi kwa kuwa hatua hiyo itaharibu sifa ya bwana Hunter na babake.
Wanachama kadhaa wa chama cha Republican walijitokeza kumtetea Trump .
Hii inaonyesha jinsi swala hilo lilivyochukua mirengo ya kichama na kugawanya watu kisiasa.
Hatahivyo mwanachama mmnoja wa Repoublic amesema kwamba anataka kujua zaidi
Bwana Trump na wafuasi wake wanadai kwamba makamu huyo wa rais wa zamani alitumia vibaya uwezo wake kuishinikiza Ukraine kutoshiriki katika uchunguzi ambao huenda ukampata na hatia mwanawe , Hunter.
0 Comments