Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Man U, kuimarika chini ya kocha wake mpya

humph the GREAT

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba kikosi chake chenye wachezaji wa umri mdogo kinaimarika kila uchao ikilinganishwa na vile walivyoanza msimu.
United imeshinda mara moja katika mechi zake tano za ligi ya Uingereza na ilihitaji penalti kuishinda klabu ya daraja la kwanza ya Rochdale katika michuano ya Carabao siku ya Jumatano.
''Sijasema kwamba itakuwa rahisi msimu huu'' , alisema mkufunzi huyo wa Man United. 
'Kutakuwa na changamoto. Tunaposhindwa mechi lazima tujiamini na kile tunachofanya''.
Kikosi hicho cha Solkjaer ambacho kilishindwa 2-0 na West Ham wikendi iliopita , kitachuana na Arsenal katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumatatu usiku.
''Utamaduni upo, hatuna tatizo na jinsi wachezaji wanachukulia kila mechi, na viwango'' , aliongezea.
''Unaweza kuona dhidi ya Astana na Rochdale, wanataka kucheza vizuri na mara nyengine wanaharakisha mashambulizi yao''.
Siku ya Jumanne, klabu hiyo ilitangaza mapato yaliovunja rekodi ya £627m.
Baada ya kuifunga Chelsea magoli manne sufuri chini ya usimamizi wa Solskjaer klabu hiyo sasa ipo nafasi ya nane katika ligi na inawafuata viongozi Liverpool kwa pointi 10 baada ya mechi sita.
''Mechi yoyote katika ligi ya Premia inaweza tukashinda na pia tunaweza kupoteza'', alisema Solskjaer.
West Ham waliilaza Man United Haki miliki ya picha Getty Images
Mara nyengine unasimama uwanjani ukiwa na furaha kwa kushinda mechi , mara nyengine umekasirika kwa kuwa umepoteza. Lazima tuonyesha picha nzuri''.
''Unaweza kuona jinsi tulivyoimarika katika safu ya ulinzi hapo ndipo tunapowekeza huku Aaron Bissaka na Harry Maguire wakiweka ulinzi wa kutosha. Hatufungwi magoli mengi''.
''Tukisonga mbele, hiyo ndio safu iliokumbwa na majeraha chungu nzima. Paul Pogba, Anthony Martial, Marcus Rashford - tumekuwa na bahati mbaya. Haisaidii unapopoteza wachezaji - vijana hawa wanahitaji kupata mfumo wa kucheza''.
Solskjaer aliwashukuru mashabiki, ambao kikosi chao kilimaliza katika nafasi tatu za kwanza katika ligi ya Premia mara moja katika kipindi cha misimu sita iliopita na kutoa wito kwa mashabiki kuendelea kuisaidia timu hiyo

Matatizo ya majeraha yanaendelea

Kijana Mason Greenwood alifunga kwa mara pili akiichezea United dhidi ya Rochdale katikati ya wiki kufuatia kukosekana kwa mshambuliaji Marcus Rashford na Martial.
Solskjaer alisema kwamba hawatawashiriikisha wachezaji wawili waliojeruhiwa dhidi ya Arsenal huku Paul Pogba akiwa katika mbio za kuwa tayari Jumatatu kufuatia jeraha la kifundo cha mguu.
Licha ya ukosefu, Solskjaer ana wasiwasi kumchezesha Green wood , 17 katika safu ya mashambulizi.
''Amethibitisha kwamba unapompata katika eneo hatari ni hatari sana'' , alisema Solskjaer.
''Kitu kilichonifurahisha kumuhusu ni kwamba hawezi kuharibu nafasi za kufunga, hivyobasi sina wasiwasi kumuhusu hata kidogo. Hatahivyo tumemzuia hatuwezi kumrusha katika safu ya mbele kila mara licha ya kwamba amethibitisha kwamba yuko tayari kila mara kucheza mbele''.
Wakati huohuo Luke Shaw amerudi katika mazoezi alisema Solskjaer na atarudi kabla ya likizo ya kimataifa mnamo mwezi Oktoba.

Post a Comment

0 Comments