MSANII wa vichekesho nchini, Anastazia Exavery maarufu kama Ebitoke amevamia mkutano wa Msanii mwezake wa Bongo Movies, Yusuph Mlela na waandishi na kutaka kupigana na mpenzi wa sasa wa Mlela.
Mlela ambaye alikuwa ameongozana na mpenzi wake mpya pamoja na msanii mwenzake ambaye ni swahiba wake wa muda mrefu, Hemmed PHD. Katika Varangati hilo, Ebitoke amesikika akisema; “Mwacheni nimwonyeshe”, huku akitukana matusi ya nguoni licha ya kudhibitwa na mabaunsa.
Ikumbukwe kuwa, Mlela alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ebitoke na sasa waneachana hivyo Mlela ana kimwana mwingine.
Kaka wa Ebitoke amesikika akimwambia Mlela, “Umemuharibia maisha mdogo wangu” huku waandishi wa habari na wasanii wenzake waliokuwepo wakibaki wameduaa.
0 Comments