Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Tanzania kuzibadili taka kuwa mkaa

humph the GREAT
chanzo BBC SWAHILI
 Jiji la Dar es Salaam ni nyumbani kwa watu wapatao milioni tano. Idadi kubwa ya watu pia inamaanisha uzalishaji kubwa wa taka.
Kwa mujibu wa ofisi ya taifa ya takwimu, Dar es salaam pekee inatarijiwa kuzalisha taka mara dufu hadi tani zaidi ya elfu 12 ikifika mwaka 2025.
Wadau wa afya na mazingira wanabuni mbinu mbalimbali za kupambana katika kupambana na utunzaji wa mazingira, hususani ongezeko kubwa la taka na uchafu wa majumbani.
Shirika la Amref Health Africa limeanzisha mradi mmojawapo unaotekelezwa na kikundi cha akinamama wanaobadilisha taka za nyumbani na kuwa mkaa.
Uchafu wa majumbani ni 75% ya taka zote zinazozalishwa jijini Dar es salaam na sehemu kubwa ya taka hizo hutupwa kiholela kutokana na kuwa na utaratibu mbovu wa ukusanyaji na uteketezaji wa taka.
Baadhi ya maeneo ya jiji haafikiki kirahisi kwa gari kama eneo la Sitakishari ambapo mradi wa Amref unapotekelezwa.
BBC imeshuhudia akinamama hao wakikusanya taka na kisha kuweka katika mashine inayogeuza uchafu huo ikewemo mabaki ya chakula kuwa mkaa.
Clara Kalepo ni mwenyekiti wa kikundi na ameiambia BBC kuwa kikundi chao kinaundwa na wajane na wathiriwa wa virusi vya ukimwi.
Mkaa taka
"Lengo ni kunyanyuana kiuchumi na kutunza usafi wa mazingira. Tunajisaidia wenyewe na wanawake wengine pamoja na watoto ambao wameathirika na ukimwi na ambao wapo katika mazingira magumu."
James Mturi meneja mradi kutoka shirika la amref health Africa anasema kuwa lengo kuu la mradi huu ni kusaidia harakati za kumaliza taka za majumbani ambazo husababisha magonjwa ya mlipuko.
"Mradi huu unalenga kutanua vipato vya hawa akinamama. Lakini pia Amref ni shirika la Afya na kupitia mradi huu tunaboresha mazingira na kupunguza uwezekano wa mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu na malaria pia maana uchafu ni mazalia ya mbu."

Mkaa huu unatengenezwa vipi?

Mkaa taka
Baada ya kukusanya taka, huwekwa kwenye tanuri na kuchomwa kitaalamu lengo likiwa ni kuondoa sumu ijulikanayo kama kabaoni.
Baada ya kuchomwa kwa saa kadhaa uchafu hugeuka na kwa majivu myeusi ambayo hukusanywa kwa pamoja na kuchanganywa na vitu ambavyo huyafanya majivu hayo kushikana katika mapande. Kitendo hicho hufahamika kwa kingereza kama binding na wanawake hao hutumia uji wa muhogo kushikanisha majivu hayo.
Baada ya kukaushwa kwa saa chache majivu hayo huwa tayari kwa matumizi ya nishati ya mkaa.
Mkaa huo ni rafiki wa mazingira kutokana na kutumia taka, lakini pia teknolojia hiyo ikiendelezwa zaidi itakuwa mbadala wa mkaa wa kawaida ambao hutokana na kukatwa kwa miti hali inayotishia ustawi wa misitu na mazingira kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments