Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Picha: Bella afanya show Ikulu katika dhifa uliyoandaliwa na Rais Magufuli kwa ajili ya Rais Kabila wa DRC

humph the GREAT
 Msanii mkongwe Zahir Ally Zorro alikuwepo kutoa burudani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Jumanne hii alimwandalia dhifa ya Taifa, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila Ikulu jijini Dar es salaam.

Shughuli hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkali wa masauti Christian Bella alikuwa mmoja kati ya wasanii ambao walialikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kusherehesha shughuli hiyo. Angalia picha.



 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo
 Mama Janeth Magufuli akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo


 Mama Salma Kikwete akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo
 Spika Mstaafu Mhe Anne makinda akimtuza mwanamuziki Christian Bella kwa kutumbuiza wimbo maarufu wa “Nani kama Mama” kwenye dhifa hiyo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila wakiagana na viongozi wastaafu Ikulu jijini Dar es salaam

Post a Comment

0 Comments