Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Raisi aongoza siku 20

humph the GREAT
RAIS wa Bolivia, Evo Morales,  amejiuzulu kufuatia maandamano ya kumshinikiza kufanya hivyo yaliyosambaa nchi nzima na kuungwa mkono na polisi na jeshi, kutokana na udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 20, mwaka huu.

Wachunguzi wa kimataifa waliokuwa wakichunguza uchaguzi ulifanyika nchini humo jana walitengua matokeo yaliyomtangaza Morales mshindi wakisema kulikuwa na udanganyifu katika upigaji kura hizo.

Morales ambaye amedumu katika nafasi hiyo tangu mwaka 2006, alikubaliana na uchunguzi huo na kutangaza uchaguzi mwingine mpya ikiwa ni baada ya kuivunja tume ya uchaguzi ya nchi hiyo huku akiwataka wananchi kuacha vurugu na kuharibu mali.

Amenukuliwa akisema  ameamua kuitisha uchaguzi mwengine ili wananchi wa Bolivia waweze kuchagua serikali mpya kwa njia ya kidemokrasia.

Kwa wiki kadhaa Bolivia imeshuhudia machafuko na ghasia dhidi ya madai ya udanganyifu katika uchaguzi wa Oktoba 20 ambapo watu watatu wameuawa na zaidi ya 300 kujeruhiwa.

Matokeo ya uchaguzi uliopita yalimpa ushindi Morales kwa asilimia 10 dhidi ya mpinzani wake Carlos Mesa na kusababisha upande wa upinzani kuishutumu serikali kwa udanganyifu.

Post a Comment

0 Comments