humph the GREAT
Idadi ya watu ambao tayari wameambukiwa virusi vya corona katika mataifa ya bara la Afrika imefikia watu 235 000.
Watu 8000 wameripotiwa kugunduliwa kuwa na maambukizi katika bara la
Afrika huku watu 200 wakiripotiwa kufariki ndani ya masaa 24.
Idadi ya visa vya maambukizi vinaripotiwa kuongezeka kama ilivyofahamisha taarifa iliotolewa Jumapili.
Idadi hiyo haikufahamisha ni taifa gani barani humo ambalo limeamthirika kwa kiasi kikubwa na maambukizi ya virusi hivyo.
Watu 201 wamefariki ndani ya masaa 24 na kufanya idadiya watu waliofariki kufikaiw watu 6281.
Watu 108 832 wamepona maambukizi ya virusi hivyo baada ya kupatiwa matibabu katika mataifa tofauti barani Afrika.
Taarifa hiyo imesema kuwa waathirika wengi wanapatikana nchini Misri.
0 Comments