​Usikose kuungana nasi kwenye matangazo yetu ya jioni tukupe habari kamili kuhusu:
👉Yanayojiri Sudan- Mwenyekiti wa bodi inayotawala Jeneralöi Abdel Fattah al-Burhan ametangaza kuwa serikali ya mpito ya nchi hiyo imevunjwa pamoja na baraza la utawala huo wa mpito.
👉Mahojiano ya kina kuhusu wanamgambo 14 wa ADF ambao wametiwa nguvuni na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
👉Asasi za kiraia nchini Tanzania, zimepinga vikali madai kwamba zimekuwa zikitumiwa na mabeberu kwa ajili ya masilahi yao binafsi.
👉Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao uliizuru Mali kutathmini hali ya usalama nchini humo, umetoa wito kwa viongozi wa serikali ya mpito kupanga tarehe ya uchaguzi
👉Mahakama moja ya Ujerumani imemhukumu mwanamke mwenye umri wa miaka 30 kifungo cha miaka 10 jela kwa hatia ya kumuacha mtoto wa miaka 5 kukaa nje akichomwa na jua hadi akafa kutokana na kiu.
0 Comments