Katika matangazo ya jioni kuna mengi tunayokuandalia na haya ni baadhi tu. Itapendeza tukiyapata maoni yako kuhusiana na ripoti hizi;
✍Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Tanzania inaridhishwa na uhusiano mzuri wa kidugu uliopo na nchi ya Burundi na kwamba itaendeleza uhusiano wake wa miaka mingi na jirani wake huyo katika nyanja mbali mbali. Haya ameyasema wakati wa ziara ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye nchini humo.
📻Mashambulizi ya ndege za jeshi la Ethiopia leo Ijumaa yameilazimisha ndege ya misaada ya kiutu ya Umoja wa Mataifa kutotua katika mji wa jimbo linalokumbwa na machafuko la Tigray.
🔦Baadhi ya wasomi pamoja na wachambuzi nchini Tanzania wameanza kuhoji mtindo mpya unaotumiwa na wanasiasa kuwataja viongozi kwa majina binafsi kuwa ndiyo wanaotoa fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za umma kama vile ujenzi wa barabara, hospitali na miradi mingine mikubwa ilhali fedha hizo zinazotumika katika miradi ni za mtoa ushuru.
▶Rais wa Somalia Mohamed Adullahi Mohamed na waziri mkuu wake Hussein Roble wamesema wamekubaliana kuharakisha mchakato wa uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu, na hivyo kumaliza mzozo unaotishia kuliingiza taifa hilo la pembe ya Afrika katika mgogoro mpya.
😷Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekutana tena leo kujadili uhamiaji katika mataifa ya Ulaya, na jinsi ya kuwazuia wakimbizi wanaoingia kutoka nchi jirani ya Belarus na pia kumuaga Kansela Angeka Merkel, mkutano huo ukitarajiwa kuwa wake wa mwisho baada ya kuiongoza Ujerumani kwa miaka 16 mfululizo.
0 Comments