Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Morrison kuombewa Ùraia wa Tanzania

​Mwandishi wa habari za michezo barani Africa kutoka Ghana, Micky Jnr amesema kama angekuwa ni Rais wa shirikisho la soka la Tanzania  TFF basi angefanya kila linalowezekana ili Bernard Morisson abadilishe uraia na kuwa Mtanzania  ili aichezee timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars. 


Micky aliongeza kuwa unapokuwa na Msuva, Bocco, Salum + Samatta pamoja na kocha mwenye mbinu na anaujua vizuri mpira basi Tanzania wangeweza kufuzu Afcon.


Micky ameongea hayo ikiwa ni siku chache tu toka  aandike kuwa anashangazwa sana, Ghana kutomwita Morisson katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ghana kwani  anaamini kwa kiwango cha Bernard Morisson anastahili kuitwa timu ya Taifa ya Ghana na angeweza kulisaidia Taifa lake la Ghana, 


Micky aliyasema hayo siku ambayo Simba SC Tanzania walicheza mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Red Arrows ya Zambia, mchezo ambao Simba waliibuka na ushindi wa goli 3-0 huku Morisson akionyesha kiwango sana katika mchezo huo.


➡️Haya wadau, wangapi wanaungana na maoni ya Micky, Morisson  apewe uraia ili acheze Stars?

Post a Comment

0 Comments